Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, June 22, 2017

IBADA YA KUWEKWA WAKFU KWA BABA ASKOFU MTEULE MCHUNGAJI BLASTON GAVILE NA KUINGIZWA KAZINI KWA MSAIDIZI WA ASKOFU MCHUNGAJI HIMID SAGGA

Pichani kutoka kushoto  ni Askofu Mteule Mchungaji Blastone Tuluwene Gavile 
akiwa na Msaidizi wa Askofu Mteule Mchungaji Himid  John Sagga
Akizungumza jioni ya leo(jana) mbele ya waadishi wa badhi ya  vyombo vya habari, Katibu Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Iringa Bwana Nayman Chavalla amesema kwa mara nyingine Dayosisi ya iringa itakuwa na tukio maalum la pili la kihistoria kwani siku ya Jumapili ya tarehe 25.06.2017 itafanyika ibada maalum ya kuwekwa wakfu Askofu wa pili wa Dayosisi hii Mchungaji  Balston Tuluwene Gavile.

Aidha katika ibada hiyo ndipo Askofu Blaston Tuluwene Gavile atamuingiza kazini Msaidi wake Mchungaji Himid John Sagga. Awali akielezea jinsi ibada hiyo itakavyokuwa alisema itaanza kwa maandamano ya Wachungaji na washarika toka usharika wa Kanisa Kuu Iringa Mjini mpaka viwanja vya Gangilonga  amabako ndiko ibada hiyo itafanyika.

Bwana  Nayman aliendelea kusema ibada hiyo inataraji kuongozwa na Mkuu wa KKKT, Askofu Fredrick Shoo akisaidana na Baba Askofu Mstaafu Dkt. Owdenburg Moses Mdegella.
Pia katika ibada hiyo viongozi mbalimbali wa Makanisa mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi, Wawakilishi wa vyama vya Kimisionari , Viongozi wa  Kiserikali, vyama vya siasa, wageni toka nchi mbalimbali, wawakilishi wa makampuni na mashirika mbalimbali watahudguria.

Katibu Mkuu aliendelea kutoa wito kwa jamii na Wakristo wote kuendelea kuliombea jambo hili.
Alimalizia kwa kusema ibada inatarajia kuanza kwa maandamanao yatakayoanza saa mbili kamili asubuhi(2:00 ASUBUHI).

Pia siku ya Jumamosi ya tarehe 24.06.2017 kutakuwa na ibada maalum ya Kushiriki Meza ya Bwana itakayofanyika katika Kanisa kuu la Kilutheri Dayosisi ya Iringa kuanzia saa 8 :00 Mchana.


MUNGU AIENDELEE KUIBARIKI DAYOSISI YA IRINGA NA TAIFA KWA UJUMLA
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment