Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, May 12, 2017

Rais mpya wa Korea Kusini apangua viongozi

Seoul, Korea Kusini. Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini aliyechaguliwa juzi, amefanya mabadiliko makubwa katika safu ya uongozi akiwateua waziri mkuu mpya, mkuu wa shirika la ujasusi, mnadhimu mkuu wa Ikulu na mkuu wa huduma ya usalama wa Rais.

Lee Nak-yon, Mkuu wa Mkoa wa Jeolla Kusini, ametajwa kuwa Waziri Mkuu katika Serikali ya Rais Moon. Uteuzi wake utawasilishwa katika Bunge la nchi hiyo na ataanza kutekeleza majukumu yake baada ya kupitishwa na wabunge.

Rais Moon pia amemteua Im Jong-seok kuwa Mnadhimu Mkuu wa Ikulu, huku Suh Hoon akiteuliwa kuchukua wadhifa wa mkuu wa shirika la ujasusi la Korea Kusini.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment