Dar es Salaam. Rais John Magufuli amemwomba Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini, mkopo kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa reli ya kisasa (Standard Gauge) kutoka Morogoro hadi Dodoma.
Rais Magufuli ambaye hakutaja kiasi cha mkopo huo, ametoa ombi hilo leo (Alhamisi) wakati wa hafla ya kutia saini mikataba ya ushirikiano kati ya Tanzania na nchi hiyo.
Amemwambia Rais Zuma kuwa hivi sasa Serikali ya Tanzania ina fedha za kujenga reli hiyo kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro, hivyo fedha zaidi zinahitajika kwa ajili ya kuendeleza ujenzi kutoka Morogoro hadi Dodoma.
Rais Magufuli amesema anaamini Serikali ya Afrika Kusini itasaidia kutoa mchango huo kutokana na historia nzuri kati ya nchi hizo mbili.
No comments
Post a Comment