May 12, 2017 Chelsea imecheza mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya West Brom ambapo bao pekee la Michy Batshuayi limeiwezesha klabu hiyo kutwaa ubingwa wa Premier League msimu wa 2016/2017 katika mchezo uliopigwa The Hawthorns.
Batshuayi alifunga bao hilo zikiwa zimesalia dakika nane mchezo kumalizika katika mchezo ambao Chelsea ilihitaji ushindi ili kutwaa ubingwa wa EPL ikifikisha point 87 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote ikibakiwa na michezo miwili kumaliza ligi.
Kwa kutwaa ushindi huo, Chelsea chini Antonio Conte imeweka rekodi ya kuwa klabu ya pili kutwaa ubingwa wa EPL mara nyingi ambapo imetwaa mata tano nyuma ya Manchester United iliyotwaa mara 13.
Chelsea imeweka pia rekodi ya kuwa klabu ya kwanza kutwaa ubingwa wa EPL siku ya Ijumaa tangu Arsenal ilipofanya hivyo katika uwanja wa Anfield 1989 huku Antonio Conte akiwa meneja wa nne kutoka Italia kushinda taji hilo baada ya Ancelotti, Roberto Mancini na Claudio Ranieri.
No comments
Post a Comment