Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, May 12, 2017

Baada ya Trump kumtumbua boss wa FBI kumeibuka haya US


Siku chache baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kumfuta kazi aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Kijasusi la Marekani FBI kuibua minong'ono kwamba Rais Trump atachungwa na Shirika hilo.
Trum amejibu minong'ono hiyo kwa kusisitiza kwamba kamwe hafanyiwi uchunguzi wowote baada ya kumfuta kazi mkurugenzi wa shirika la ujasusi la FBI.

Bwana Trump aliambia chombo cha habari cha NBC kwamba ilikuwa uamuzi wake pekee kumsimamisha kazi James Comey.

Bwana Comey alikuwa akiongoza uchunguzi kuhusu madai ya Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani uliokamilika mbali na uwezekano kwamba kulikuwa na mawasiliano kati ya, maafisa wa Trump na Urusi wakati wa kampeni.

Bwana Trump ameutaja uchunguzi huo kuwa unafiki mkubwa madai yaliopingwa na Mrithi wa Comey.

Katika mahojiano yake ya kwanza tangu alipomfuta kazi mkurugenzi huyo , Bwana Trump aliambia NBC siku ya Alhamisi kwamba alimuuliza bwana Comey iwapo alikuwa akimchunguza.

Nilimwambia iwapo inawezekana unaweza kuniambia, Je Ninachunguzwa? Aliniambia ,huchunguzwi.

''Najua sichunguzwi'', Bwana Trump alimwamabia aliyekuwa akimhoji, akirejelea madai aliyotoa katika baraua ya Jumanne ya kumfuta kazi bwana Comey.
Rais huyo pia alipinga maelelezo ya ikuu ya Whitehouse kwamba alimfuta bwana Comey baada mapendekezo kutoka maafisa wakuu wa wizara ya haki.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment