Dar es Salaam. Balozi wa Korea nchini Song Geum-young amesema serikali yake ipo tayari kuisaidia Tanzania katika teknolojia ya kisasa ya kusafisha maji.
Akizungumza wakati wa mkutano uliowakutanisha wataalam wa maji wa Korea na Tanzania Geum-young jijini hapa leo alisema nchi yake imebobea kwenye teknolojia hiyo na ipo tayari kuishirikisha Tanzania endapo itakuwa tayari.
Mkurugenzi wa Huduma bora za Maji kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Nadhifa Kemikimba alisema serikali iko tayari kupokea teknolojia hiyo na huenda ikawa msaada kukabiliana na changamoto ya maji yasiyo salama.
"Tutaupitia mradi wao kama itaonekana teknolojia hiyo inafaa nina imani serikali itakuwa tayari kuipokea."alisema
Inaelezwa kuwa teknolojia hiyo ina uwezo wa kuondoa bakteria,uchafu na chumvi iliyopo kwenye maji.
No comments
Post a Comment