Writen by
sadataley
1:53 PM
-
0
Comments
Mchezo wa kimataifa wa Raundi ya
Pili kati ya Young Africans ya Dar es Salaam, Tanzania na Mouloudia Club
D’Alger ya Algeria unatarajiwa kufanyika leo Jumamosi Aprili 8, 2017
kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam ambako utachezeshwa na
waaamuzi kutoka Rwanda.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), waamuzi hao ni Louis
Hakizimana ambaye atakuwa mwamuzi wa kati akisaidiwa na Theogene
Ndagijimana akiwa mshika kibendera wa mstari wa kulia na Jean Bosco
Niyitegeka ambaye atakuwa mshika kibendera mstari wa kushoto.
Mwamuzi wa akiba ambaye pia
atakuwa anatokea Rwanda ni Ruzindana Nsoro wakati Kamishna wa mchezo
atakuwa Ata Elmanan Hassan Osama kutoka Sudan. Waamuzi hao pamoja na
Kamishna wa mchezo wamefikia Hoteli ya Urban Rose iliyoko Mtaa wa
Jamhuri, katikati ya jiji la Dar es Salaam, Tanzania.
Wapinzani wa Young Africans ambao
ni Alger waliingia jana usiku saa 3.30 kutoka Algeria kwa ndege maalumu
ya kukodi na kufikia Hoteli ya Holiday Inn. Kwa mujibu wa kanuni, leo
Ijumaa Aprili 7, mwaka huu saa 10.00 jioni watafanya mazoezi kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mchezo huo muhimu kwa Young
Africans kusonga mbele kama ilivyotokea msimu uliopita kwa kuifunga
Sagrada Esperanca ya Angola na kutinga hatua ya makundi, viingilio
vimepangwa kuwa Sh 30,000 kwa VIP ‘A’; Sh 20,000 kwa VIP ‘B’ na ‘C’
wakati mzungunguko itakuwa ni Sh 5,000.
Akizungumzia mchezo huo, Kocha
msaidizi wa Young Africans, Juma Mwambusi alisema: “Wachezaji wa Yanga
wako na morali wa hali juu na kikubwa tunawaomba Watanzania kujitokeza
kwa wingi kuishangilia timu hii kwa sababu ni klabu pekee iliyobaki
ikiiwakilisha nchi.”
…………………………………………………………………………….
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA
No comments
Post a Comment