Writen by
sadataley
10:03 AM
-
0
Comments
Na Mahmoud Ahmad Arusha
MAGEUZI ya Katiba ya Chama cha Mapinduzi,pamoja na kanuni zake yanalenga kukidhi mahitaji ya sasa ya CCM mpya na Tanzania mpya kwa kuteremsha madaraka ngazi za chini kuliko na wanachama ili kukimarisha chama .
Hayo yameelezwa April 5 na Naibu katibu mkuu CCM bara Lodrick Mpogolo, alipokuwa akizungumza na halmashauri za ccm za wilaya ya Arusha , Meru na Arusha DC, kwenye ukumbi wa chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha.
Amesema kikubwa kilichopo sasa ni kuimarisha matawi na mashina ya chama cha mapinduzi ambapo kuanzia sasa balozi lazima awe na wanachama 150 wa ccm kwenye maeneo yao .
Mpogolo, amewaagiza wajumbe hao wa halmashauri hizo kuwa lazima wakaandae mashina hayo kuanzia sasa ili chama kiweze kushinda kwenye chaguzi mbalimbali za serikali ambazo hushirikisha pia vyama vingine vya kisiasa
Amesema atarejea tena Arusha kufanya ziara ya kukagua utekelezaji wa maagizo hayo ya kuwepo mashina na kukagua uhai wa chama ambapo atataka kuona uhalisia wa wanachama na daftari la wanachama kwenye mashina yote.
Amewaambia kuwa mageuzi hayo ya ndani ya chama yameeondoa majungu, kupakana matope kwa kuwa ccm ya sasa ni ya mtumaini kwa wananchi hivyo majungu na fitina hazina nafasi tena ndani ya chama .
Amesema kuanzia sasa Makatibu wa ngazi ya mikoa na wilaya ni marufuku kukaa ofisini bali watumie muda mwingi kutoka kwenda kutafuta wanachama ili kuwezesha chama kupata ushindi na si vinginevyo na ambae hawezi kutembelea wananchi kusikiliza kero na kutafuta wanachama wapya ajiondoe kwenye utumishi wa chama .
Mpogolo,amesema chama kinahitaji ushindi kwenye uchaguzi wowote utakaojitokeza mbele yake na katibu akikaa ofisini ushindi hautapatikana hivyo hahitajiki na hana nafasi ndani ya chama.
Makatibu wote wa chama na jumuia zake watapimwa kwa utendaji wao na uongezaji wanachama wapya kuanzia matawi hadi wilaya lengo ni kupata viongozi bora na wenye mapenzi na chama chao.
Kuhusu uchaguzi wa viongozi mbalimbali, amewaonya makatibu kutokuwa kikwazo kwa kuwazuia wanachama kujaza fomu za kugombea uongozi ngazi yeyote ile ,aidha amewataka makatibu kuacha mara mja mtindo wa kuwa na wagombea wao kwa kuwa ccm inataka kiongozi ambae atawaunganisha wanachama, wananchi na chama chao.
Ametanabaisha kuwa wala makatibu wasiwachagulie wanachama viongozi bali jukumu la kuchagua viongozi ni la wanachama kwa utashi wao na sio kwa shinikizo.
Kuhusu wapiga debe na mawakala wakati wa uchaguzi ndani ya chama Kuanzia sasa ni marufuku mawakala na wapiga debe ndani ya ccm wakati wa uchaguzi ,amesema anashangaa mawakala na wapiga debe ambao huibuka wakati wa uchaguzi na kuhoji hutokea wapi kwani hata kwenye katiba na kanuni haziwatambui na pia sio wajumbe hivyo kuanzia sasa ni marufuku kuwepo kwao.
Amesema sababu ya kupotea kwa majimbo ya ubunge mkoani Arusha ni kutokana na kuwepo viongozi maslahi binafsi ambao walikuwa hawafanya kazi ya mtu badala ya kazi za chama hivyo kuanzia sasa tunahitaji kupata kiongozi mwenye maslahi ya chama na anayefanya kazi za chama na sio za mtu .
Kuhusu mapato ya chama amezitaka kamati za siasa kuhakikisha zinasimamia mapato na mapato hayo yatumike kukiimarisha chama na sio mtu binafsi,Pia kamati za siasa zote zifanye ukaguzi wa mapato na waliokula fedha hizo watashughulikiwa ,waliokula fedha za uchaguzi mkuu 2015 nao watashughulikiwa.
Awali Katibu wa ccm,mkoa wa Arusha, Elias Mpanda, alisema kuwa makatibu wote ambao ni wapya mkoani wamepelekwa Mkoani Arusha ili kufanya kazi za chama na sio za mtu.
Ameongeza kuwa tayari chama cha mapinduzi kimekamilisha semina za uchaguzi wa ndani ya chama ngazi zote na wanachama wameeleweshwa kuhusu mageuzi yaliyofanywa ndani ya katiba na kanuni zake.
No comments
Post a Comment