Writen by
sadataley
11:53 AM
-
0
Comments
Hali ilivyokuwa baada ya Lori kuwagonga watu nchini Sweden
Lori limegonga mkusanyiko wa watu katikati ya jiji la Stockholm nchini Sweden na kusababisha maafa na majeruhi.
Nina Odermalm Schei, msemaji wa wa idara
ya Inteljensia nchini humo ameliambia Shirika la Habari la Ufaransa AFP
kuwa watu wamepoteza maisha lakini hakutoa idadi.
Waziri Mkuu Stefan Lofven amesema tukio hilo ni la kigaidi na kusababisha vifo vya watu watatu.
Ripoti zinasema kuwa Lori hilo lilikuwa limeibwa baada ya kuwasilishwa kwa wamiliki wa hoteli moja.
Walioshuhudia tukio hilo la Ijumaa jioni wanasema lilikuwa na kuogofya sana.
Uongozi wa mji huo umetangaza kusitishwa kwa safari za treni katika mji huo.
Hakuna kundi ambalo limejitokeza kudai kuhusika na shambulizi hilo.
No comments
Post a Comment