Writen by
sadataley
11:51 AM
-
0
Comments
Mkuu
wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa kwenye mazoezi na wananchi
wa kijiji cha Tosamaganga pamoja na mwanachama wa club ya Tosamaganga
sports club
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akicheza Mpira wa kikapu kuashiria kuwa anapenda Mpira wa kikapu
Na Fredy Mgunda,Iringa
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela aliwaomba wananchi kuendelea kufanya mazoezi kwa ajili ya kuimalisha afya zao pamoja kuujenga uchumi wa nchi hii.
Tukiendelea
kufanya mazoezi tutapunguza sana kupata magonjwa mbalimbali kwa kuwa
tuna kuwa tunaimalisha afya na kujenga miili yetu lakini hii itasababisa
wananchi kujituma kufanya kazi kwa nguvu na morali mpya kila mwanzo mwa
wiki kwa kuwa wanakuwa na nguv,stamina na akili Mpya kutokana mazoezi
ya mwisho mwa Juma.
“Kwa
mfano mimi saizi nipo sawa kiakili kutokana na haya mazoezi maana bila
haya mazoezi nisinge kuwa vizuri kiaafya,saizi naweza kufanya kazi kwa
masaa mengi kutokana na hili zoezi la Leo sasa nawaomba wananchi na
viongozi mbalimbali kufanya mazoezi ili kuongeza ufanisi kazini”alisema
Kasesela
Aidha
Kasesela aliwashukuru wananchi wa Tosamaganga sports club kwa
kuanziasha club ya Tosamaganga ambayo inamichezo mingi kama mpira wa
miguu,mpira wa pete,riadha,na mpira wa kikapu hivyo naomba wananchi
wengine waanzishe vitu kama hivi ili Wilaya nzima iwe inafanya mazoezi
kwa kuimalisha Afya.
Kasesela
amewataka viongozi wa kata,kijiji,mtaa,na tarafa kuanzisha mazoezi huku
waliko ili kupanua wigo wa eneo kubwa la watu kufanya mazoezi ili
kuimalisha afya zao na kupunguza kunyemelewa na magonjwa mbalimbali
ambayo yamekuwa yanapunguza nguvu kazi za taifa katika kujenga uchumi wa
taifa.
“Hii
ni moja ya club ambayo nimeizindua ambayo itatuongezea wigo wa sehemu
za kufanyia mazoezi ya kuimalisha afya zetu na kuipa moyo serikali
kupanua wigo wa maeneo ya kuafanyia mazoezi” alisema Kasesela
Nao baadhi ya viongozi wa club ya Tosamaganga sports club walimushukuru mkuu wa Wilaya kwa kukuza Michezo katika Wilaya ya Iringa na kuongeza ufanisi wa kazi hasa makazini kwa kuwa ndio jadi ya kukuza uchumi katika mkoa wa Iringa.
Nao baadhi ya viongozi wa club ya Tosamaganga sports club walimushukuru mkuu wa Wilaya kwa kukuza Michezo katika Wilaya ya Iringa na kuongeza ufanisi wa kazi hasa makazini kwa kuwa ndio jadi ya kukuza uchumi katika mkoa wa Iringa.
Chanzo: Fullshangwe Blog
No comments
Post a Comment