Rais wa Marekani, Donald Trump
Washington, Marekani. Imeripotiwa kuwa mazungumzo ya simu kati ya Rais wa Marekani, Donald Trump na Waziri Mkuu wa Australia, Malcolm Turnbull yaliingia doa jana, wakati viongozi hao walipokuwa wakibadilishana mawazo kuhusu suala la wakimbizi.
Waliingia kwenye mabishano kuhusu sera mpya ya Trump ya kupiga marufuku raia kutoka mataifa saba kuingia Marekani, huku akikataa kupokea wakimbizi kutoka Syria.
Vyombo vya habari viliripoti kwamba, Trump alisema tangu aingie madarakani mazungumzo hayo ni ya kwanza kumchukiza tangu aingie madarakani na kusababisha akate simu.
Viongozi hao, walikuwa wakijadili kuhusu makubaliano ya watu wanaoomba hifadhi Australia kuhamishiwa Marekani.
Baada ya tukio hilo kusambaa kwenye vyombo vya habari, Trump aliamua kuandika kwenye mtandao wake wa Twitter akibainisha hoja zilizoibuliwa na Turnbull akisema: “Nitafanya uchunguzi kuhusu makubaliano hayo”.
No comments
Post a Comment