Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, February 3, 2017

MAKUBALIANO YA KIKAO CHA KIMATAIFA CHA UHAMASISHAJI WA AFYA NA LISHE KWA VIJANA

LISHE 1
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto kwa kushirikiana Micronutrient Initiative Tanzania iliandaa Kikao cha kimataifa cha uhamasishaji wa Afya na Lishe kwa vijana kilichoanza februari 1, kimefika tamati leo hii februari 3 katika ukumbi wa kimataifa wa Mwaalimu Julius Nyerere,
 Dhamira kuu ya kikao hicho ilikuwa ni kupitia mwongozo  Mpya wa WHO wa kuwapa wasichana Madini Chuma na vitamini ya Foliki Asidi mara moja kwa wiki ili kupambana na tatizo la upungufu wa damu kwa kundi hili.
Katika kikao hicho kilichohudhuriwa na nchi zaidi ya tano zikiwemo Senegal, Kenya, Ethiopia,Canada,wenyeji Tanzania, taasisi mbali mbali na mashirika yakimataifa ikiwemo WHO, washiriki wote wamekubaliana kwa pamoja ni lazima kuboresha Afya na lishe ya kundi hili kwakuwa ni kundi ambalo limesahaulika kwa kipindi Kirefu katika jamii.
Habari kwa hisani ya Mjengwa Blog
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment