Writen by
sadataley
8:55 PM
-
0
Comments

Kaimu Mtendaji Mkuu wa PSPTB Bw. Godfrey Mbanyi akifunga mafunzo ya siku tatu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya (JKCI) jijini Dar es salaam leo , yaliyokuwa na lengo la kujenga uwezo kwa watendaji wa taasisi hiyo katika mchakato wa Ununuzi wa Umma, akifafanua zaidi wakati akifunga mafunzo hayo amewaasa wataalamu hao wa Ununuzi kuvaa joho la Uzalendo wa nchi ili kulitumikia vyema taifa na watanzania kwa ujumla
Ametolea mfano kuwa “Unaweza kutumia vibaya fedha kidogo kama Milioni tatu hivi, lakini fedha hiyo ni muhumu sana kwa maisha ya wananchi kwani kama ingetumika vizuri huenda ingeweza kununua vitanda kadhaa kwa ajili ya wazazi kujifungulia kule kijijini na wananchi wakapata unafuu wa maisha kwa kupungumza matatizo yanayokabili sekta ya afya, Hivyo ni vyema nawaasa kuwa kila mnapofanya kazi zenu muwafikirie watanzania kwanza kabla ya kijifikiria ninyi kwanza.
Akitoa neno la Shukurani Dk. Tulizo Shemu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete amesema mafunzo hayo yamekuwa muhimu sana kwao na wamepata uelewa jinsi ya kufanya Ununuzi wa Umma na wameomba kama itapatikana nafasi nyingine ni muhum kupata mafunzo zaidi ili kuzidi kuelewa mabadiliko ya sheria ya Ununuzi wa Umma.
Katika Picha kulia ni Ally Songoro Mkurugenzi wa Maendeleo ya Taaluma PSPTB na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Profesa Mohamed Janabi.(P.T)

Bw. Hamis Tika Mwanasheria wa PPAA akitoa mada katika mafunzo hayo yaliyomalizika leo kwenye Taasisi ya JKCI.

Ally Songoro Mkurugenzi wa Maendeleo ya Taaluma PSPTB akizungmza jambo katika mafunzo hayo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Profesa Mohamed Janabi akitoa shukurani zake kwa PSPTB wakati wa kufunga mafunzo hayo.

Mratibu Mkuu wa Utafiti na Ushauri PSPTB Bw. Amos Kazinza na Afisa Mwandamizi wa Mahusiano ya Umma na Masoko Bi. Shamimu Mdee wakifuatilia mambo kadhaa wakati wa mafunzo hayo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Profesa Mohamed Janabi akisisitiza jambo wakati wa kufunga mafunzo hayo.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia wakati wa ufungaji mafunzo.

Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa katika picha ya pamoja.
No comments
Post a Comment