Writen by
sadataley
4:21 PM
-
0
Comments
Na Exuper Kachenje, Mwananchi
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku amekionya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuwa kipo hatarini kupoteza madaraka katika uchaguzi mkuu ujao, iwapo kitafanya makosa na kuendekeza ubinafsi na utawala wa kiimla unaotokana na utamaduni wa rushwa na matumizi mabaya ya mali za umma.
Butiku ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba, alisema kuwa iwapo chama hicho kitasahau kuwa
kinaiongoza nchi kwa mujibu wa Katiba ya nchi ambayo sasa Watanzania
wanataka iandikwe upya na kuendelea kukumbatia maovu kinaweza kuondolewa
madarakani.
Alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam, Jumatano
wiki hii katika mahojiano maalumu na gazeti hili ambapo alizungumzia
mambo mbalimbali.
“…Kosa moja la msingi ni CCM kusahau misingi ya
Katiba ya chama chao na Katiba ya nchi. Watanzania wengi wanaikubali
Katiba ya CCM na Katiba ya nchi, lakini ambayo wanasema itazamwe upya,
iandikwe Katiba Mpya,” alisema Butiku.
Huku akisisitiza, Butiku alisema: “CCM wakisahau
kwamba madaraka yao ni ya kikatiba, wakadhani yapo katika utawala wa
kiimla unaotokana na kuimarisha utamaduni wa rushwa na matumizi mabaya
ya mali na rasilimali za taifa, watapoteza madaraka kama siyo leo ni
kesho.”
Alifafanua kuwa hali hiyo itaikumba CCM kwa kuwa ndiyo kanuni ya maisha ya binadamu akisema:
“Vyama vyote tawala vilivyosahau masilahi ya
wananchi wake, demokrasia, uhuru na haki, vikakumbatia uovu vinaanguka.
Huo siyo utabiri wangu binafsi, bali historia itawahukumu.”
Butiku alitoa mfano akieleza: “Mfumo wa kibabe
zaidi wa makaburu wa Afrika Kusini, uliangushwa na wasio na viatu. Nani
anaweza kujenga ubabe wa sura kama ule wa makaburu, nani ataruhusu? Ni
muhimu CCM nayo ijitazame.”
Rushwa
Alisema kuwa alipoondoka madarakani, Baba wa Taifa
Mwalimu Julius Nyerere alisema taifa linanuka rushwa hali ambayo imeota
mizizi hata sasa.
“…Leo rushwa ni kawaida, ni mfumo wa kuuza na
kununua uongozi, kama taifa mkifika hapo ni hatari. Mkishanunua uongozi
basi mmekwisha. Mkijenga mfumo huo, mnaondoa haki.
Ikiwa kura yako imekuwa biashara umekwisha, hakuna
ushirikiano tena kati ya kiongozi aliyenunua nafasi na mwananchi. Hapo
mnajenga kundi la viongozi la wafanyabiashara wa kura katika uchaguzi,
mnajenga mfumo wa raia kuwa maskini.”
“Raia wakiuza haki yao na kununua hakutakuwa na taifa lenye
utulivu. Wanunua kura wajue ni vita, siku moja wauza kura wataamua
kuwaondoa nao watagoma kwa kuwa walinunua uongozi, hapo damu itamwagika,
watu watauana.
Wanyonge hawapotezi haki ya unyonge wao, unaweza kuiangusha CCM…
No comments
Post a Comment