Writen by
sadataley
6:37 PM
-
0
Comments
Mchungaji Mwasumbi akiwa mahakamani mwaka jana. ©Global Publishers |
Hatimaye Mchungaji Daniel Mwasumbi ambaye mwaka jana alihukumiwa na
Mahakama ya Wilaya ya Mbeya kifungo cha miaka thelathini (30) jela Julai
mwaka 2013 kwa tuhuma za ubakaji hapo jana tarehe 3 Juni ameachiwa huru
na Mahakama kuu kanda ya Mbeya huku akiwa anatetewa na wakili wa
kujitegemea Benjamini Mwakagamba mbele ya jaji Atuganile Ngwala, huku
upande wa serikali ukiwakilishwa na Prosista Paul.
Kwa mujibu wa WAPO Radio FM 98.1 kupitia kipindi cha Yaliyotokea
kinachorushwa saa moja usiku, ripota kutoka mkoani Mbeya bwana Ezekiel
Kamanga ambaye alifika mahakamani hapo, anasema kwa upande wa utetezi
wakili Benjamini Mwakagamba aliwasilisha sababu saba ambazo zilikuwa
zikiomba mahakama hiyo kumwachia huru kutokana na hakimu kukosea
kuzingatia moja ya mashahidi ambaye alikuwa ni shahidi wa kwanza.
Ameongeza kuwa pili ni kuwa hakimu alikuwa ameegemea ushahidi wa upande
mmoja tu hivyo mahakama haikuwa na haki ya kumfunga kifungo hicho cha
miaka thelathini . La tatu ni kuwa hakimu alitumia maoni yake binafsi
kumfunga mshtakiwa hali ambayo ni kinyume cha sheria. Sababu ya nne
ambayo ilitolewa na upande wa utetezi ni kutumika kwa kivuli cha kadi ya
kliniki hali ambayo haikuwa ni halali kuweza kuwakilisha kama upande wa
ushahidi.
Lakini sababu nyingine ni kuhusu kuchelewa kwa vipimo vya DNA kutumwa
jijini Dar es Salaam huku pia sababu nyingine ikielezwakuwa kubwa ni
kukosewa au kutozingatia muda wa kesi hiyo mara baada ya kufikishwa
polisi kutumia mda mrefu tangu kukamatwa, kwani ilichukua takribani
miezi minne ndipo alipokamatwa mtuhumiwa hali ambayo mahakama ilitilia
shaka na hivyo kwa upande wake jaji Atuganile Ngwala kuamua kumwachia
huru kutokana na sababu hiyo ni kwamba hivi sasa mchungaji Daniel
Mwasumbi atakuwa huru ambapo kesi hiyo ya rufaa namba 59 ya mwaka 2013
ikimalizikia hapo, ali iliyopelekea watoto wa Mchungaji Daniel Mwasumbi
kuangua kilio cha furaha mahakamani.
Taarifa zinasema kwa upande mwingine magereza wanasikitika kuachana na
Mchungaji Mwasumbi kwa hali aliyokuwa ameionyesha kwa siku za hivi
karibuni, kwani hata WAPO Radio ilipomtembelea, alionekana mwenye
kukubaliana na hali aliyoko, huku pia akikubalika sana gerezani hapo kwa
kuhubiri injili, ambapo pia alikuwa kiongozi wa ibada gerezani huku
wengine wakiachiwa huru kwa maombi aliyokuwa akiwafanyia na wengine
wakimpokea Yesu.
Mara baada ya kuachiwa huru Mchungaji Daniel Mwasumbi hakuweza
kuzungumza lolote kwani alichukuliwa na gari la magereza ili kwenda
kukamilisha taratibu za kuachiwa huru lakini kwa upande wa watoto wake
ilikuwa ni furaha na kumshukuru Mungu kwa kile kilichotokea huku wakidai
kuwa alifungwa kwa hila na njama za baadhi ya watu ambao walikuwa
wakipinga huduma yake ambayo alikuwa anaifanya katika kanisa la EAGT
eneo la Iwambi.
Habari na www.gospelkitaa.co.t
No comments
Post a Comment