Writen by
sadataley
6:40 PM
-
0
Comments
Kifungo ©Stand up for the truth |
Imeanika wazi kwamba taifa la Nigeria ndio nchi ambayo wakristo nchini
humo wanaishi kwa mateso makubwa, ikilinganishwa na nchi nyingine
duniani. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na shirika la kimataifa la
Open Doors kupitia kitengo chake cha World Watch List kuanzia kipindi
cha November 1, 2012 hadi Machi 31, 2014, Nigeria imeshika namba moja
ikifuatiwa na mataifa ya Syria, Misri, Jamhuri ya Afrika ya Kati,
Mexico, Pakistan, Colombia, India, Kenya na Iraq.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo ambayo imeegemea takwimu za namna makanisa na
mali za wakristo zilivyoteketezwa, na maasi dhidi yao mathalani kupigwa,
utekwaji nyara, ubakaji, kukamatwa hovyo na hata kulazimishwa ndoa,
inaonyesha kuwa Nigeria inaongoza ikiwa na matukio 2,073 huku Syria
ikiwa na matukio 1,479. Mataifa mengine yanayofuatia ni pamoja na
Jamhuri ya Afrika ya Kati 1,115, Pakistan 228, Misri 147, Kenya 85, Iraq
84, Mnyanmar (Burma) na Sudan ikiripotiwa kuw ana 33, na Venezuela
ikiwa na matukio 26.
"Kujitangaza kwamba ni mkristo kwenye mataifa haya ni kama kujitoa mhanga, unajiweka hatarini"
Na kati ya mauaji 5,479 ya wakristo duniani kote, Nigeria, Syria na
Jamhuri ya Afrika ya Kati wameunda asilimia 85 ya jumla hiyo, huku
takwimu zikikadiria kuwa kuna wakristo 322 wanaouwawa kila mwezi.
Korea ya Kaskazini, taifa ambalo linaongoza kwa mateso ya wakristo
kwa mwaka 2014, halijaorodheshwa kwenye 'kumi bora' kutokana na
kinachoendelea nchini humo kuwa cha siri mno kiasi kwamba unaweza usijue
kilichopo, kulinganisha na muundo wa utafiti huo ambao umebeza taarifa
za mitandao, vyombo vya habari na maofisa walioko ngazi za chini kwenye
jamii mbalimbali.
Taarifa fupi kutoka utafiti huo.
1. Nigeria;
Taifa hili limegawanyika katika maeneo mawili, kusini na kaskazini,
ambapo kusini mwa nchi hiyo kumekaliwa na wakristo wengi, wakati huko
kaskazini kuna idadi kubwa ya waislamu. Matukio mengi yameripotiwa
kutokea eneo la kaskazini ambapo maeneo yake mengi yanatawaliwa na
sheria za kiislamu, ambapo hata hivyo kundi la Boko Haram limejikita
zaidi kuwabadili watu kuwa waislamu, wakishambulia wakristo silaha
mbalimbali ikiwemo mabomu na hata utekaji nyara. Sababu nyingine
inaelezwa kuwa ni uwepo wa kundi la kiislamu la Fulani (Muslim Fulani
Herdsmen) ambao huvamia maeneo ya wakristo na kuwapora ardhi.
2. Syria;
Idadi ya wakristo nchini humu inaripotiwa kuwa chache, na katika kipindi
cha kuandaliwa ripoti ya utafiti huu, ianoyesha kuwa wakristo wengi
wameuwawa kutokana na vita inayoendelea nchini humo, msimamo wa waislamu
wenye itikadi kali waliopo kwenye kamundi yanayoshiriki vita ya wenyewe
kwa wenyewe nchini humo na pia hata kuwekwa kati kwa wakristo baina ya
makundi ya Shia na Sunni yanayohasimiana. Aidha wakristo wameendelea
kuwa kwenye hatihati nchini humo kutokana na kukisiwa kuunga mkono
utawala wa Bashar al-Assad.
3. Misri;
Taifa hili ambalo lipo kwenye mpito, lina idadi kubwa ya wakristo kwa
mwamvuli wa kikoptiki (Coptic Orthodox Christians), linatatizwa na
mashambulizi mbalimbali ambayo yalizidi kushamiri mara baada ya
kuondolewa madarakani Rais Mohamed Morsi mnamo July 2013. Ambapo kikundi
cha Muslim Brotherhood pamoja na makundi mengine yamehusika na
mashambulizi hayo ikiwemo kuchoma makanisa na mali za wakristo nchini
humo, na pia mauaji.
4. Jamhuri ya Afrika ya Kati;
Japokuwa taifa hili lina idadi kubwa ya wakristo kulinganisha na makundi
mengine, ripoti inaonyesha kuwa kundi la Séléka limekuwa likilenga
jamii ya wakristo, ikiwemo vijiji, ambapo lengo lao kuu ni kutaka
kulibadili taifa hilo kuwa la kiislamu. Licha ya kwamba mateso
yameripotiwa, matukio mengine huenda kuwa yameachwa kutokana na kutopata
usahihi wa taarifa.
5. Mexico;
Ukabila na rushwa imeripotiwa kuwa chanzo kikuu cha mashambulizi kwa
wakristo nchini humu, ambapo licha ya wingi wao, wakristo wamelazimika
kuishi kwa mashaka kutokana na maeneo waliyopo kuongozwa na mila ambazo
mtu akikengeuka huweza kushambuliwa. Na kundi kuu ambalo limekumbwa na
athari hizi ni jamii ya Wapentekoste, Walutheri na pia 'Presbyterian'
Habari na http://www.gospelkitaa.co.tz
No comments
Post a Comment