Writen by
sadataley
10:46 AM
-
0
Comments
Na Daniel Mjema na Sharon Sauwa, Mwananchi
Dodoma. Kuna kila dalili kwamba homa ya makadirio ya matumizi ya Wizara ya Maji na ile ya Nishati na Madini inazidi kupanda na jana wabunge wa CCM walikutana kwa dharura ili kunusuru bajeti hizo.
Habari kutoka ndani ya kikao hicho zinasema,
Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliwatangazia wabunge hao kuwa Serikali
imekubali kuiongezea Wizara ya Maji Sh100 bilioni kufidia pengo la Mwaka
wa Fedha 2013/2014.
Kadhalika wabunge hao waliambiwa kuwa Serikali pia
imekubali kutoa Sh50 bilioni kwenda Wakala wa Umeme Vijijini (Rea)
ambazo zilikusanywa na Hazina lakini hazikupelekwa kama taratibu
zinavyoelekeza.
Taarifa za uhakika kutoka Hazina, zinaonyesha kuwa
katika Mwaka wa Fedha 2013/2014, Rea ilipaswa kupokea Sh123.7 bilioni
lakini hadi kufikia Machi mwaka huu, ilikuwa imepokea Sh79 bilioni. Kama
ilivyokuwa katika bajeti ya Maji, kitendo cha Hazina kutoipatia Rea
fedha hizo kwa wakati kuliibua hasira za wabunge wengi ambao walijipanga
kukwamisha Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini.
Kwa upande wa Maji, katika Mwaka wa Fedha wa
2013/2014, Wizara ya Maji ilikuwa ipewe Sh184 bilioni kutekeleza miradi
ya maji lakini hadi kufikia Machi mwaka huu, Serikali ilikuwa imetoa
Sh86 bilioni.
Habari za uhakika zilizolifikia gazeti hili
zinasema kuwa kutolewa kwa fedha hizo ambazo awali ilionekana
zisingetolewa, kulitokana na jitihada kubwa zilizofanywa na Kamati ya
Bunge ya Bajeti inayoongozwa na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew
Chenge.
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba alikiri
kwamba wizara hizo zitapatiwa fedha hizo lakini akasema siyo nyongeza
bali ni utekelezaji utoaji wa fedha za mwaka 2013/2014.
“Maji tutawapa kama bilioni 50 hivi na Rea pia
tutawapa kiasi kama hicho na kwa upande wa Rea tutakuwa tumetoa fedha
zote kwa asilimia 100 ila Maji watapata fedha zote kabla ya kuisha kwa
mwaka fedha,”alisema.
Serikali kwa Mwaka wa Fedha wa 2013/2014 ina
upungufu wa Sh1.8 trilioni za bajeti ya maendeleo hali iliyosababisha
baadhi ya wizara kupata asilimia kati ya 19 na 30 ya fedha za maendeleo.
Fedha za escrow
Habari zaidi zinasema ndani ya kikao hicho
kuliibuka sakata la kashfa ya Sh200 bilioni ya Akaunti ya Escrow ya
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambapo baadhi ya wabunge walitaka Waziri wa
Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo awajibike.
Hata hivyo, Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola ndiye
aliyemwokoa Profesa Muhongo baada ya kusema kwa vile suala hilo tayari
limekabidhiwa vyombo vya kiuchunguzi, ni vyema wabunge wakasubiri ripoti
hiyo.
Kwa habari ziadi ingiahttp://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Serikali-yaiongezea-Wizara-ya-Maji-Sh100-bil/-/1597296/2329942/-/10r1pn0z/-/index.html
Kwa habari ziadi ingiahttp://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Serikali-yaiongezea-Wizara-ya-Maji-Sh100-bil/-/1597296/2329942/-/10r1pn0z/-/index.html
No comments
Post a Comment