Writen by
sadataley
6:21 PM
-
0
Comments
Dar es Salaam. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka juzi aliwekwa kitimoto na wabunge waliotishia kuondoa shilingi kukwamisha bajeti ya wizara yake kiasi cha kumlazimisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuingilia kati na kuokoa jahazi.
Pinda aliokoa jahazi baada ya mbunge wa Kigamboni,
Dk faustine Ndungulile kukataa kurudisha shilingi akieleza kuwa
Serikali haijashirikisha wadau katika mradi huo utakaogharimu Sh11.7
trilioni utakapokamilika.
“Nimeona kuna tatizo la elimu kwa umma kuhusu
mradi huu na ushirikishwaji,” alisema Pinda baada ya mbunge wa viti
maalum (CCM), Esther Bulaya kumuomba aingilie kati ili kuondoa aibu kwa
Serikali.
“Serikali tunaomba tuachiwe suala hili. Wizara itaanza kutoa elimu kuhusu mradi huu.”
Awali Tibaijuka, ambaye alikuwa na kazi ya kujibu
tuhuma za ufisadi wa kutumia madaraka vibaya katika mgogoro wa Chasimba
na kiwanda cha saruji cha Wazo Hill jijini Dar es salaa, alijitahidi
kupangua hoja za kambi ya upinzani na wakati mwingine kumshambulia
mbunge wa Kawe, Halima Mdee aliyeshikia bango mgogoro wa wananchi wa
Chasimba na kiwanda cha saruji cha Wazo Hill.
Tibaijuka, ambaye alikuwa mkurugenzi wa Shirika la
Makazi ya Umoja wa Mataifa (UN-Habitat), baadaye alisema anakubaliana
na mawazo ya wengi kuhusu hali na mazingira ya mji wa Kigamboni uliopo
jijini Dar es Salaam hivyo kwa kuwa kuna kasoro na kwamba suala la
ushirikishwaji linawezekana.
Sakata hilo, ambalo lilionekana kumnyima raha
Waziri Tibaijuka kadri mjadala ulivyokuwa unaendelea, lilitokea wakati
Bunge lilipokaa kama kamati kupitisha vifungu vya bajeti hiyo ya Sh88.9
bilioni.
Mbunge wa Kigamboni, Dk Ndungulile aliondoa
shilingi katika mshahara wa waziri akipinga namna Serikali
inavyoutekeleza mradi wa uendelezaji wa wa mji wa Kigamboni bila ya
kuwashirikisha wakazi wa Kigamboni.
Dk Ndungulile alisema kuwa wananchi hawashirikishwi katika mradi huo wala hawaelewi hatima ya malipo ya fidia ya nyumba zao.
Badala yake, mbunge huyo alisema, wananchi
wanalazimishwa kununua hisa kwa ajili ya umiliki wa mradi huo, kitu
ambacho alikipinga.
“Suala la kuwa na hisa si la lazima ni hiari,
kwanza waziri anazidi kuwachanganya wananchi wa Kigamboni ambao
hawajaelimishwa kuhusu suala hilo, hivyo naondoa shilingi katika bajeti
yako,” alisema Dk Ndungulile.
Mbunge huyo aliungwa mkono na wabunge wengine
akiwamo mbunge wa viti maalum (CCM), Esther Bulaya, mbunge wa Temeke,
Zuberi Mtemvu na mbunge wa viti maalumu (CCM), Zarina Madabida.Kwa habari zaidi ingiahttp://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Prof-Tibaijuka-asalimu-amri-Kigamboni/-/1597296/2331324/-/fdskv8z/-/index.html
No comments
Post a Comment