Writen by
sadataley
6:20 PM
-
0
Comments
Kampuni ya Google inatarajiwa kuzindua huduma ambayo,
itawawezesha raia wa Ulaya kuomba viambatanishi vya mitandao yenye
taarifa kuhusu maisha yao kufutwa
Google ambao hutumiwa kwa ukubwa duniani
kutafuta taarifa imesema kamati ya wakurugenzi wakuu na wataalamu wa
kujitegemea wataunda mpango wa muda mrefu kushughulikia maombi hayo ya
watu kutoka Ulaya.Hatua hiyo inajiri baada ya mahakama ya haki Ulaya kuamua kwamba viambatanishi vya data za zamani au zisizo muhimu za watu zinapaswa kufutwa iwapo watu wataomba hivyo.
Mkurugenzi mkuu wa Google, Larry Page amesema kampuni hiyo itafuata hukumu hiyo ya Ulaya lakini ameonya huenda ikaathiri ubunifu na ikafurahisha nchi zenye watawala wakandamizaji.
No comments
Post a Comment