Writen by
sadataley
6:24 PM
-
0
Comments
Kwa muda mrefu sasa, serikali imekuwa ikijinadi kuwa ni sikivu kwa matatizo ya wananchi wake.
Hiyo imetokea kuwa kaulimbiu muhimu kwa viongozi
wake wengi kwa ngazi mbalimbali, wakiwamo mawaziri kila wanapozungumzia
masuala mazito ya jamii.
Kwa kutumia kaulimbiu hiyo, mara nyingi Serikali
imekuwa ikijinadi kuwa ipo makini, inawatumikia wananchi au Watanzania
wote kwa umakini na uadilifu.
Lakini, kwa kuangalia majadiliano na mijadala
mingi ambayo imekuwa ikiendelea ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano
linaloendelea na vikao vyake mjini Dodoma, usikivu huu wa Serikali kwa
hakika unatia shaka.
Tunasema kauli hizi zinatia shaka hasa kwa sababu
inaonekana maoni na ushauri unaoonekana kuwa mzuri na wenye tija
unaotolewa bungeni, umekuwa hautiliwi maanani na wakati mwingine kubezwa
na hata kufanyiwa mzaha.
Ushauri huo ambao hutolewa ama na wabunge au
kupitia maoni ya kamati za Bunge na mawaziri kivuli wa kambi ya
upinzani, umekuwa ukitolewa majibu mepesi na pengine kubinafsishwa na
matokeo yake yamekuwa ni kushambuliwa kwa msemaji au mtoaji ushauri.
Hii imetokea karibu katika wizara zote zilizowasilisha hotuba zao za makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2014/15.
Mawaziri hao walitumia muda mwingi kushambulia
kambi ya upinzani, wasemaji wao na kutotolea majibu mapungufu ambayo
yalibainishwa na kamati husika za wizara hizo.
Matukio ya hivi karibuni ni yale yaliyomuhisisha
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa na Wizara wa Maliasili na Utalii ambao
walitumia muda mwingi kushambulia maoni au hoja za wabunge, hasa wa
upinzani, na hivyo kutotoa majibu yanayolenga kuondoa utata kwenye
masuala yaliyohojiwa.
Hatutaki kuamini kuwa maoni, maswali na hoja
zinazotolewa dhidi ya serikali zote si sahihi na zinastahili kubezwa na
kutolewa majibu yasiyoondoa utata unaotakiwa uwekwe bayana.
Mawaziri na Serikali hawana budi kutambua kuwa
wabunge ni wawakilishi wa wananchi na mambo wanayohoji wanafanya kwa
niaba ya wananchi na huweza kuhoji kwa sababu wanatumia muda wao mwingi
kufanya tafiti kwa ajili ya kupata uwezo wa kuihoji na kuisimamia
serikali.
Kwa hiyo, tunadhani Serikali haina budi kujitazama
upya jinsi inavyopokea na kufanyia kazi ushauri na maswali
yanayoibuliwa na wabunge.
Kwa habari zaidi ingiaMawaziri acheni jeuri, ubabe kuweni wasikivu
Kwa habari zaidi ingiaMawaziri acheni jeuri, ubabe kuweni wasikivu
No comments
Post a Comment