Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, May 30, 2014

SHANGILIENI ARUSHA KUACHIA DVD MPYA WIKI MBILI ZIJAZO


Kwaya maarufu nchini ya Tumaini Shangilieni kutoka kanisa la Kianglikana parokia ya Mtakatifu James Kaloleni jijini Arusha, inatarajia kuachia DVD yake mpya iitwayo 'Nisamehe' tarehe 8 mwezi June mwaka huu, katika ibada itakayofanyika kanisani kwao Arusha.

DVD hiyo ambayo inasubiriwa kwa hamu na wapenzi wa muziki wa injili nchini, itakuwa inavionjo na madhari ya kipekee hasa kutokana na kwaya hiyo kuwa na wadada wapya ambao wameongoza baadhi ya nyimbo kwa umaridadi lakini pia baadhi ya picha katika DVD hiyo, zilirekodiwa nchini Afrika ya Kusini  wakati kwaya hiyo ilipotembelea nchini humo mwishoni mwa mwaka jana.

Tumaini ni moja kati ya kwaya kongwe ambazo zinaendelea kuhimili mitego ya shetani kwa kuendelea kusimama katika wito ilioitiwa lakini pia umoja na upendo katikati ya wanakwaya wa kwaya hiyo umewafanya kumiliki vyombo vya kisasa, mabasi mawili ya kusafiria, duka kubwa la kanda ambalo pia limekuwa likiiongezea kwaya hiyo kipato katika kusukuma gurudumu la injili.

Aidha kwa wale wapenzi wa kwaya hiyo, wanaweza kupata miito ya simu kwa kununua nyimbo za Tumaini kupitia kampuni ya Tigo, album ambayo inapatikana kwasasa 'Unishike'. Namna ya kupata miito na wimbo kuchagua angalia picha chini. Wakati huo huo kwaya hiyo inatarajia kuelekea mkoani Tabora wiki inayofuatia baada ya uzinduzi kwa ajili ya huduma.








    Habari na Gospel Kitaa
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment