Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, April 16, 2014

Meli yenye watu 460 yazama Korea.K

Ferry yenye abiria 460 ikizama Korea Kusini.
Oparesheni ya uokozi inaendelea kufuatia ishara za dharura zilizoripotiwa kutoka meli moja iliyobeba takriban abiria 460 katika pwani ya Korea Kusini.
Maafisa wanasema kuwa walinzi wa pwani hiyo wanatumia, meli za wanamaji wa Korea pamoja na ndege za uokoaji kuwaokoa watu waliokuwa katika meli hiyo.
Jeshi la wanamaji likishirikiana na maafisa wanaolinda usalama katika bahari ya rasi ya Korea wanasema watu wengi wamefanikiwa kuolewa.Shughuli zinaendelea hivi sasa kuokoa zaidi ya abiria 460 wa ferry hiyo .
Maafisa wanasema walipokea habari kuwa meli hiyo imepata matatizo ikiwa imebeba idadi kubwa ya wanafunzi ikitoka Incheon iliyoko kwenye visiwa vya kifahari vya Jeju .
Waokoaji wamewanusuru tayari abiria 160 huku wengine waliosalia wakishauriwa waruke baharini iliwaokolewe.
Walioshuhudia wanasema kulisikika kishindo kikubwa kabla ya ferry hiyo kuanza kuzama zaidi ya kilomita 20 kutoka ufukweni.

Shughuli ya uokoaji bado inaendelea.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment