Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, April 12, 2014

JK, marais wastaafu, Pengo kumkumbuka Sokoine

Kaburi la aliyekuwa Waziri Mkuu na Mbunge wa Monduli, Marehemu Edward Moringe Sokoine 
Na Peter Saramba, Mwananchi
Arusha. Rais Jakaya Kikwete na Kiongozi wa Kanisa Katoliki nchini, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ni miongoni mwa watu mashuhuri wanaotarajiwa kuhudhuria maadhimisho ya miaka 30 ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, hayati Moringe Sokoine yanayofanyika leo nyumbani kwake Monduli Juu, Wilaya ya Monduli mkoani Arusha.
Mmoja wa watoto wa hayati Sokoine, Namelok alisema jana kuwa maandalizi yote yamekamilika na kwamba kumbukumbu hiyo inayotarajiwa pia kuhudhuriwa na viongozi wakuu wastaafu wakiwamo marais wastaafu wa awamu ya pili na tatu, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa.
Namelok ambaye pia ni mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (viti maalumu), alisema kuwa familia kwa kushirikiana na Serikali imeandaa misa maalumu kumwombea hayati Sokoine zitakazofanyika katika mikoa ya Dodoma, Morogoro, Dar es Salaam na Arusha (Monduli).
“Pamoja na misa pale eneo la Dakawa ajali ilipotokea, pia kutakuwa na misa nyingine Dodoma, Dar es Salaam katika Kanisa la Mtakatifu Peter na Joseph na nyumbani Monduli Juu,” alisema Namelok
Maadhimisho hayo pia yatapambwa na mbio za nyika zitakazoanzia eneo la Monduli Jeshini na kumalizikia Monduli Juu ambako ndiko kijiji anakotoka Hayati Sokoine.
Hayati Sokoine alifariki dunia kwa ajali ya gari iliyotokea eneo la Dakawa, mkoani Morogoro Aprili 12, mwaka 1984.
Habari zaidi kuhusu kumbukumbu hiyo soma makala maalumu Uk.., 12 25,26,27,28
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment