Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, April 12, 2014

Wakenya waliotekwa 2011 waokolewa

Raia wa Kenya waliotekwa nyara na kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Al Shabaab mwaka mwaka 2011 nchini Somalia, wameokolewa na wanajeshi wa Kenya
Majeshi ya AMISOM yamekuwa yakipambana na wapiganaji wa Al Shabaab na kudhibiti baadhi ya maeneo waliyokuwa wameyateka
Wakenya hao walikuwa wanafanyia kazi mashirika ya misaada ya kibinadamu .
Awali walikuwa chini ya uangalizi wa majeshi ya Kenya ambao ni sehemu ya kikosi cha Umoja wa Afrika kilichopo nchini Somalia AMISOM.Daniel Njuguna ambaye alikuwa akifanya kazi katika shirika la Madaktari wasio na mipaka Medecins Sans Frontieres MSF na James Kiarie wa Shirika la Care International, walikaguliwa kiafya na walitarajiwa kupelekwa Nairobi.
Kenya ilipeleka majeshi yake kwenda nchini Somalia mwaka 2011 kujiunga na AMISOM kufuatia matukio ya utekaji nyara yaliyokuwa yakiendeshwa na wapiganaji wa Al shabaab katika mipaka ya nchi hiyo na Somalia.
Majeshi ya AMISOM yakishirikiana majeshi yale ya serikali ya Somalia yamekuwa yakiendesha mapambano dhidi ya wapiganaji wa Al Shabaab ambao wanafadhiliwa na kundi la kigaidi la al Qaeda linaloshikilia maeneo ya kusini na katikati mwa Somalia.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment