“Miaka 33 iliyopita, alikuwa mhubiri wetu hadi tukaja kupata revival, nakumbuka mwaka 1977 tulikuwa na wakristo takribani 5,000 lakini kwa hivi sasa tuna takribani wakristo 80,000 – hii imetokana na mchango mkubwa ambao Dakta Kulola amechangia.”
Haya ni maneno ambayo Askofu Niyungeko Samuel wa kanisa la Pentekoste nchini Burundi anaieleza Gospel Kitaa katika mahojiano maalum kutokana na msiba wa Askofu Moses Kulola.
“Mara kadhaa nimekuja nchini Tanzania, na pia nimekuja mara kadhaa kumchukua ilia je kuhubiri.”
Askofu Niyungeko anaeleza tukio la yeye kufunga safari hadi Tanzania kumfuata Askofu Kulola kwa ajili ya kwenda kuhubiri nchini humo, licha ya kwamba kipindi hicho kulikuwa na tafrani ikiwemo purukushani za vita ya Kagera, lakini Kulola alikubali na kwenda nae ambapo mkutano mkubwa sana ulifanyika, na kisha matokeo yake wengi wakamgeukia Mungu.
Hakika Kanisa la Pentekoste Bujumbura litamkumbuka kwa mengi, maana ni kama pia amewalelea hadi wakakua na kusimama kwa miguu yao. Anastahili kuitwa si tu baba, bali pia ni babu wa wasiohesabika.
Yawezekana wengine bado hawajajua umuhimu wa kazi aliyofanya Askofu Kulola na hata kufikia kumdharau, lakini hakika ni kwamba mbegu alizopanda, zinaendelea kutoa matunda, kazi yake bado yaonekana, na sio ya kufutika leo wala kesho.
No comments
Post a Comment