Writen by
sadataley
7:14 PM
-
0
Comments
![]() |
| Askofu Mkuu wa Redeemed Gospel Church, Dakta Arthur Kitonga |
Rais wa shirikisho la uinjilisti Afrika kwa kanda ya Afrika Mashariki, Askofu Dakta Arthur Kitonga, ambaye pia ni mwanzilishi na mkuu wa kanisa la Redeemed Gospel Church Inc, ameeleza kuguswa na kifo cha Askofu Dakta Moses Kulola, na kusema kwamba Kenya pia imepoteza mtu muhimu sana katika injili
Katika mahojiano maalum na Gospel Kitaa, Dkt Kitonga amemuelezea Askofu Kulola kama mtu muhimu ambaye aliihubiri injili na kusisitiza umoja na kusameheana. Kufuatia hiyo, Askofu Kitonga ameitakia heri EAGT ipate kusonga mbele bila kutetereka, kwani kufikia kuwa na makanisa zaidi ya 4,000, sio jambo dogo.
Shirikisho la Uinjilisti la Afrika pia litamkubuka Askofu Kulola kutokana na kwamba amekuwa mtu wa karibu sana na pia amekuwa mshauri wao, na hivyo kwa hivi sasa, hakika pengo litakuwepo na litaonekana.
“Nilikuwa mchanga sana kihuduma, ndio nikawa karibu nae”, Dakta Kitonga anaiambia Gospel Kitaa na kuendelea “Baba ndio jina sahihi kwa mimi kumuita, hakunizaa kiroho, lakini ana roho ya ubaba, kwangu mimi ni baba.”
Gospel Kitaa pia imefahamu kuwa Askofu Kulola ameelezwa kuheshimika kwenye taifa la Kenya kuliko hata Maaskofu wazawa wa huko, nah ii ni kutokana na mchango wake katika injili, na kwamba kila anapokuwa na safari ya huko, basi huwa kuna gumzo na kujiandaa kutokana na namna alivyokuwa akiieneza injili bila haya na kwa kujituma.
Mbali ya hayo, Askofu Dakta Kitonga ameieleza Gospel Kitaa kuwa kwa pamoja yeye na Dakta Kulola walimsimika kiongozi mmojawapo wa kanisa la redeemed jijini Mwanza, na hiyo ndo ikawa mara ya mwisho kwa Askofu Kulola kusimika kiongozi, hakupata nafasi nyingine hadi mauti ikamkuta.

No comments
Post a Comment