Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, September 6, 2013

Viongozi wa dunia watofautiana kuhusu Syria

Viongozi wa dunia wanaokutana katika mji wa St. Pettersburg nchini Urusi kwa kongamano la mataifa ishirini yenye uwezo mkubwa wa kiviwanda G20 wameshindwa kukubaliana kuhusu hatua zinazofaa kuchukuliwa dhidi ya Syria huku msemaji wa serikali ya Urusi akisema kuna mgawanyiko mgkubwa kuhusiana na swala hilo.
Viongozi wa nchi za Magharibi wakubali kumuunga mkono Obama wakati Urusi imekataa azimio la kuvamia Syria
Duru zinaarifu kwamba viongozi wa Uingereza, Ufaransa, Uturuki na Canada wanaunga mkono azimio la rais wa Marekani Barrack Obama kuishambulia Syria kijeshi kutokana na madai ya serikali ya rais bashar al Assad kutumia silaha za kemikali.

Wakati huo huo Balozi wa Marekani katika Umoja wa mataifa Samantha Power ameikashifu Urusi kwa kuzuia umoja wa mataifa kuichukulia Syria hatua.Lakini rais wa Urusi, Vladimir Putin, amesema kuwa bado haijabainika ni upande upi ulitumia silaha hizo.
Umoja wa mataifa unasema kuwa unahitaji dola bilioni tatu unusu zaidi kukabiliana na tatizo la wakimbizi kutuka Syria hadi mwisho wa mwaka huu.
Afisa mkuu wa shirika la umoja huo kuhusu haki za kibinadamu,Valerie Amos, ameiambia BBC kwamba mataifa wafadhili yanastahili kutathmini upya mchango wao na kuyataka kuwa wakarimu zaidi.
Umoja wa mataifa unakadiria kwamba watu milioni mbili wamekimbia Syria na wengine milioni nne wanaishi maisha ya ukimbizi nchini Mwao.
Valarie Amos anasema masaibu ya Wasyria yana uzito mkubwa kuhusu usalama ana amani ya dunia kutokana na idadi kubwa ya watu wanaokimbia kufuatia shambulizi la silaha za kemikali.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment