Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, September 5, 2013

Bunge la Kenya kujadili kujiondoa ICC

Naibu rais wa Kenya William Ruto
Wabunge nchini Kenya wanatarajiwa kukutana kwa dharura hii leo kujadili ikiwa nchi hiyo itajiondoa kwenye mahakama ya kimataifa ya ICC au la.
Hatua hii ya wabunge inakuja zaidi ya wiki moja kabla ya kuanza kwa kesi dhidi ya naibu Rais wa Kenya Williiam Ruto kuhusiana na ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2008Ruto anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu.
Rais Uhuru Kenyatta pia anatarajiwa kufika katika mahakama hiyo mwezi Novemba kuhudhuria kesi dhidi yake.
Wawili hao wanashtakiwa kwa kuhusika na ghasia za baada ya uchagu
zi mwishoni mwa mwaka 2007.
Msemaji wa ICC ameambia BBC kuwa kesi hiyo itaendelea hata ikiwa Kenya itajiondoa kwenye mkataba wa Roma uliopelekea kuanzishwa kwa mahakama hiyo.
Bwana Fadi El Abdallah, alisema kuwa itachukua karibu mwaka mmoja kwa mchakato wa nchi yoyote yoyote ile kujiondoa kutoka katika mahakama ya ICC na hii bila shaka inaathiri tu kesi zilizokuwa mbele ya mahakama hiyo kwa wakati huo.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment