Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, September 1, 2013

WATU 1,000 WAVAMIA NA KUVUNJA KANISA NA KUSHAMBULIA WAUMINI

Jengo la kanisa, kabla na baada ya shambulizi. ©Gospel for Asia, kupitia Christian Post
Takriban kundi la watu 1,000 wamevamia na kuvunja jengo la kanisa ambalo lilikuwa kwenye ujenzi, baada ya kucheleweshwa kwa kipindi cha miaka miwili kutokana na hofu ya shambulio kwenye kijiji kimoja kaskazini mwa India, na kisha kuwashambulia waumini waliokuwa eneo hilo.

Tukio hilo limeripotiwa kutokea  Jumapili, iliyopita ambapo wavamizi walisikika wakisema kuwa hawataki kuona jengo la kanisa hilo kwenye maeneo yao.

Wavamizi hao ambao wako kinyuma na dini ya kikristo, walivamia eneo hilo na kukwea juu ya jengo hilo na kisha kuezua nondo zilizokuwa zimeksukiwa hapo kwa muda mfupi, jambo ambalo Mchungaji Tanvir, anasema kuwa hakika ni shetani alikuwa kazini kutokana na namna walivyoezua nondo hizo ilhali zilikadiriwa kuwa na uzito wa tani moja.

Kwa mujibu wa tovuti ya Gospel for Asia, eneo hilo ambalo linakabiliwa na changamoto ya kueneza injili, linategemea maombi ya waamini popote pale walipo, ili basi amani itawale na hofu kutoweka miongoni mwa waliovasmiwa, ambapo siku hiyo pamoja na kufanikiwa kutoroka mikononi mwa watesi wao, hawakurudi majumbani mwao kutokana na uhofia usalama wao.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment