Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, September 1, 2013

ANGALIA PICHA ZA IBADA YA KUUAGA MWILI WA ASKOFU KULOLA JIJINI DAR ES SALAAM

Jeneza lililohifadhi mwili wa marehemu, Askofu Mkuu, Moses Kulola. ©Philemon Rupia/WAPO Media
Kutokana na maelfu ya watu kujitokeza kwa wingi kumuaga Askofu wa Maaskofu, Baba/Babu wa kiroho kwa wengi nchini, zoezi la kuaga mwili wake limesitishwa kwa muda kutokana na idadi ya watu kuelemea eneo la tukio, kwenye kanisa la EAGT Temeke.

Gospel Kitaa imeshuhudia kila mtu akijitahidi kw akadri ya uwezo wake kufika eneo ambalo jeneza lipo ili apate kutoa heshima zake za mwisho, lakini umati wa watu kufanyika kizuizi, ambapo pia hitilafu ya mitambo iliyopelekea vipaza sauti kuzimika, imechangia kupungua kwa ufanisi wa mawasiliano eneo hilo.

Huenda zoezi likasitishwa kabisa iwapo mambo hayatokaa sawa, ila kwa kadri waratibu wanavyoweka mambo sawasawa, nafasi ya kuendelea kuaga inatumainiwa zaidi na kila aliyeacha
shughuli zake kutokana na umuhimu wa hayati kwenye maisha yao.

Picha za tukio lote zitakujia hivi punde, endelea kutembelea Gospel Kitaa kwa mengi zaidi.Picha wakati wa ibada ya heshima kwa mwili wa aliyekuwa askofu mkuu wa kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania(E.A.G.T) iliyofanyika katika kanisa hilo Temeke jijini Dar es salaam ambapo makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Ghalib Bilal alikuwa miongoni mwa viongozi walioshiriki katika ibada hiyo.

Wabunge wa chama cha Mapinduzi mh. mchungaji Getruda Rwakatare pamoja na Asumpta Mshama wakitia saini kitabu cha wageni.


Askofu mkuu wa WAPO Mission International Sylvester Gamanywa akimfariji mke wa marehemu.

Askofu mkuu wa kanisa la Ufufuo na uzima, Josephat Gwajima akitoa salamu zake " Shujaa amerejea nyumbani"
Mtume na nabii Anthony Lusekelo a.k.a Mzee wa Upako akizungumza.

Mheshimiwa Philip Mangula akizungumza mengi kuhusu walivyofahamiana na marehemu, aliwagusa wengi alipomalizia kwa kuimba pambio la iende mbele injili.


Mheshimiwa Mangula na mkewe wakitoa salamu zao za rambirambi kwa mke wa marehemu.




Mheshimiwa mbunge wa Nkenge mkoani Kagera na mchungaji msaidizi wa kanisa la Mito ya baraka ambaye pia ni mama mzazi wa waimbaji wa kundi la J'sisters akitoa salamu zake za rambirambi.
Mheshimiwa Dkt, mchungaji Getruda Rwakatare akitoa salamu zake.

Balozi na mkuu wa mkoa wa Dar mstaafu Mh. Mary Chipungahelo akitoa salamu.
Waziri Theresia Uvinza akizungumza. 

Meza kuu ilisheheni.

Askofu Zachary Kakobe akizungumza maneno yaliyowagusa wengi hasa ujumbe wake kwa kanisa la E.A.G.T pamoja  na mitume na manabii kuacha tamaa ya fedha.

Watoto, wajukuu na ndugu wakiwa katika huzuni.

Mtume Onesmo Ndegi wa Living water Makuti Kawe akitoa salamu.
Makamu wa Rais akitia saini kitabu cha maombolezo.
Mjane mama Moses Kulola akiwa mwenye huzuni kubwa.

Meza kuu.


Makamu wa Rais akitoa salamu na pole kwa wafiwa.
Mwimbaji wa injili Abihudi Misholi akiimba wimbo maalumu wa kumuaga askofu Kulola msibani hapo.


Katibu mkuu wa Chadema, Dkt Wilbroad Slaa akitia saini kitabu cha maombolezo.


Akizungumza na waombolezaji msibani hapo.

Makamu wa Rais wa aliyezibwa na mpiga picha akitoa heshima zake za mwisho. Shukrani brother Herry Malekela kwakuwezesha tukio hili kwenda hewani.

Habari picha na Gospel Kitaa
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment