Writen by
sadataley
9:00 AM
-
0
Comments
Rais Obama akizungumza na waandishi wa habari Ikulu ya Marekani, anayemfuatia ni Rais wa Lithuania, Bi Dalia Grybauskaite, na makamu wa Rais, Joe Biden. ©Reuters/Kevin Lamarque |
Hofu imezidi kutanda kuhusiana na hatua ya Marekani kuendelea kutilia mkazo uamuzi wa kutumia nguvu za kijeshi dhidi ya taifa la Syria, linalotuhumiwa kutumia silaha za na kuua takriban watu 1,429.
Rais Obama ameweka msimamo wake wazi Ijumaa tarehe 30, wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa mojawapo ya jukumu kama kiongozi duniani ni kuhakikisha kuwa kama kuna utawala wowote utakaotumia silaha ambazo zimekatazwa kimataifa dhidi ya watu wao, ikiwemo watoto, basi yapasa wawajibike.
"Tukio la serikali ya Syria pia linahatarisha maslahi ya usalama wa taifa wa Marekani", Obama alisema na kuongeza kuwa, "inatishia marafiki na washirika kama Israel na Uturuki na Jordan, na kwamba silaha za sumu zinaweza kutumika katika siku za karibuni"
"Serikali ya Marekani haitaki dunia ipoozwe, na changamoto kubwa tuliyonayo hapa ni kwamba watu wengi wanadhani kuna haja ya mtu kufanya kitu kuhusu hili, na hakuna anayetaka kulifanya." Alisema Obama ambaye pia ameeleza kuwa amechoshwa na vita.
Kwa upande wake, Askofu Richard Pates, ambaye ni kiongozi wa kamati ya maaskofu ya kimataifa ya haki na amani ameiasa Marekani kutazama uwezekano wa kusitisha vita badala yake.
"Uwezekano wa usuluhishi wa kidiplomasia unaonekana kuwa mzuri zaidi ya uharibifu na maumivu na kuteseka na vifo, hasahasa kwa wananchi wasio na hatia ambao wataumizwa na hatua ya Marekani kuttumia nguvu za kijeshi". askofu Pates aliiambia National Catholic Reporter.
Askofu Pates pia amemuandikia barua katibu wa taifa, John Kerry, akiitaka serikali ya Marekani kushirikiana na serikali nyingine ili kupata suluhu ya kusitisha vita, na kujadiliana kwa kina ikiwemo kuhusu misaada ya kibinadamu, na pia kuijenga jamii ya Syria iliyo shirikishi na yenye kulinda haki za wananchi wote ikiwemo wakristo na jamii nyingine ndogondogo.
Christian Post imeripoti
No comments
Post a Comment