Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, September 1, 2013

Viongozi watoa ushuhuda Kulola alivyowasaidia

Mdhamini wa Makanisa ya EAGT, John Mfuko akitoa heshima za mwisho mbele jeneza lenye mwili wa Askofu Mkuu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania(EAGT), Dk Moses Kulola jijini Dar es Salaam. Picha na Salim Shao. 
Na Beatrice Moses, Mwananchi
Dar es Salaam. Ibada ya kuaga mwili wa Askofu Mkuu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania(EAGT), Dk Moses Kulola (83) ilichukua sura mpya baada ya viongozi kadhaa wa Serikali nchini, kufunguka na kutoa siri za mafanikio yao kwa maombi yake ikiwemo kupata uwaziri.
Viongozi hao ni pamoja na Paul Kimiti ambaye alikiri mbele ya maelfu ya waombolezaji kwamba maombi ya Askofu huyo, yalimpa mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupata uwaziri mara mbili.
“Nakumbuka aliniombea tena ofisini kwangu wakati huo nikiwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, mbele ya bendera za taifa nilipiga magoti mbele ya mtumishi wa Mungu alikuwa anatembea na Yesu, kweli kila goti litapigwa kwa Yesu, kwa maombi yake nilifanikiwa kuwa waziri kwa vipindi viwili, ilibaki nusra niupate na uwaziri Mkuu,” alisema Kimiti akifuatiwa na kelele za kushangiliwa.
Kimiti amewahi kuwa Waziri wa Ajira na Maendeleo ya Vijana na Waziri wa Kilimo na Biashara, kati ya mwaka 1995 na mwaka 2000.
Kwa upande wake, Mchungaji Getruda Rwakatare ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu, alisema Askofu Kulola alikuwa ni baba yake wa kiroho na kwamba alimtambua baada ya ndoa yake kuwa na mgogoro.
“ Alinifariji sana, aliniombea nakumbuka kuna wakati nilimweleza jinsi mateso yalivyoendelea katika ndoa yangu, aliniambia kama mume wako anakupiga au kukutesa tambua hakutesi wewe bali Yesu aliye ndani yako, maneno yale yalinitia nguvu nikabadilika nikawa mtumishi wa Mungu hadi leo naye akawa ananiita nabii Debora,” alisema Mchungaji Rwakatare.
Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Advera Senso akiwasilisha rambirambi ya Sh 2,000,000, alisema kuwa jeshi hilo limepoteza kamanda wa kiroho na kimwili ambaye walikuwa wanamtumia kutokana na mahubiri yake katika kuzuia matukio ya uhalifu ikiwemo ya kikatili ya kukata viungo vya albino.
Makamu wa Askofu wa EAGT, Asumwisye Mwaisabila akitoa salamu zake kwenye ibada hiyo, aliwataka viongozi wote wa makanisa ya kiroho kumaliza tofauti zaoili kumuenzi Askofu Kulola ambaye alikuwa na upendo wa pekee.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment