Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, July 2, 2013

Wake wa marais kuzungumzia nafasi ya mwanamke Afrika

Wake za marais kutoka mabara mbalimbali duniani, leo wanakutana kuzungumzia majukumu muhimu ya wake za marais katika kutetea elimu, afya na uchumi wa wanawake duniani.
Mkutano huo ulioandaliwa na Taasisi ya Rais wa zamani wa Marekani, George W. Bush utawakutanisha wakwe za marais, maofisa wa Serikali, taasisi binafsi na wanataaluma kujadili utendaji bora wakati wa ushirikiano wa taasisi binafsi na Serikali.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana, majadiliano hayo yatawanufaisha wanawake, kisiasa, kiafya na kiuchumi na hatimaye kujenga jamii imara.
Rais Bush na mke wake, Laura watazungumza kwenye mkutano huo ambao utahudhuriwa na mke wa Rais Barack Obama, Michelle, Salma Kikwete, Roman Tesfaye wa Ethiopia na Maria Da Luz wa Msumbiji.
Wake wengine wa marais ni Panehupifo Pohamba wa Namibia, Sia Nyama Koroma wa Sierra Leone, Janet Museveni wa Uganda na Christine Kaseba wa Zambia.
Wengine ni Cherie Blair, Mwasisi wa Mfuko wa Wanawake wa Cherie Blair na Nancy Brinker, Mwenyekiti wa Mpango wa Kupambana na Saratani. Mengine yatakayozungumzwa ni masuala ya usalama, mbinu za kupambana na saratani ya shingo ya kizazi na maziwa, elimu na kuwainua wanawake kibiashara kupitia mafunzo na teknolojia.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment