Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, August 21, 2018

Watu 103 wakamatwa katika maandamano ya kupinga kukamatwa Bobi Wine Uganda


Maandamano yazuka Kampala kupinga kukamatwa mbunge Bobi Wine
Image captionMaandamano yazuka Kampala kupinga kukamatwa mbunge Bobi Wine
Polisi nchini Uganda inasema imewakamata watu 103 katika maandamano yaliozuka kupinga kukamatwa kwa mbunge wa upinzani Robert Kyagulanyi au Bobi Wine pamoja na wabunge wengine kadhaana wanaharakati nchini Uganda.
Inaarifiwa pia mtu mmoja ameuawa katika purukushani hiyo.
Vikosi vya usalama nchini Uganda vilizima maandamano kwenye mji mkuu hapo jana Kampala kupinga kukamatwa kwa Bobi Wine .
Waandamanaji wamechoma moto magurudumu ya magari, wanarusha mawe huku pia wakiweka vizuizi vya barabarani.
Bobi Wine alikamatwa na kushtakiwa kwenye mahakama ya kijeshi wiki iliyopita kufuatia madai kuwa alikuwa anamiliki silaha kinyume cha sheria.
Wengi wanayaona mashataka hayo kama yaliyochochewa kisiasa.
Bobi Wine alikamatwa na kushtakiwa kwenye mahakama ya kijeshi wiki iliyopitaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBobi Wine alikamatwa na kushtakiwa kwenye mahakama ya kijeshi wiki iliyopita
Wanajeshi na polisi walionekana wakiwa juu ya magari wakipita kati kati mwa mji. Sehemu nyingine za mji wa kampala maafisa wa usalama wamefyatua risasi hewania na kurusha vituo machozi kutawanya waandamanaji.
Misukosuko inaongezeka mjini Kampala kufuatia kukamatwa kwa mbunge Bobi Wine. Ripoti zimeibuka kuwa aliteswa akiwa mikononi mwa wanajeshi. Rais Yoweri Museveni amekana madai kuwa Bobi Wine alijeruhiwa.
Waandamanaji wanachoma moto magurudumu ya magari, wanarusha mawe huku pia kuweka vizuizi vya barabarani.
Image captionWaandamanaji wanachoma moto magurudumu ya magari, wanarusha mawe huku pia kuweka vizuizi vya barabarani.
Watu kadhaa wamekamatwa akiwemo mwandishi wa habari wa Reuters aliyekuwa akifuatilia ghasia hizo.
Wiki iliyopita Bobi Wine 32, na watu wengine walishtakiwa baada ya kampeni za kuelekea uchaguzi mdogo eneo la Arua kaskazini mwa nchi. Polisi wanasema walikuwa wamewaongoza wafuasi wao kushambulia msafara wa Rais Museveni.
BBC
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment