Writen by
sadataley
12:10 PM
-
0
Comments
Kiongozi wa kanisa katoliki Papa Francis yuko katika upande wa wahanga wa zaidi ya mapadre 300 waliofanya unyama wa unyanyasaji mkubwa kingono nchini Marekani wanaoshutumiwa kuwafanyia unyanyasaji zaidi ya watoto 1000.
Unyama huo ulifanyika katika kiondi cha miongo saba, yameeleza makao makuu ya kanisa Katoliki mjini Vatican.
Wahanga watambue kuwa papa yuko upande wao, imesema taarifa ya Vatican baada ya ripoti mbaya ya jopo la mahakama nchini Marekani kuchapishwa siku ya Jumanne inayoelezea hatua za kuficha madhila hayo zilizofanywa na kanisa Katoliki.
"Kuna maneno mawili yanayoweza kueleza hisia zinazokabili uhalifu huu wa kutisha, aibu na masikitiko. Papa anachukulia kwa dhati kazi ya jopo la mahakama pamoja na ripoti iliyotoa. Papa analaani bila kiasi unyanyasaji kingono watoto wadogo. Unyanyasaji ulioelezwa katika ripoti ni uhalifu na kiroho ni wa kukemewa. Vitendo hivyo ni usaliti wa imani ambayo imewapora wale waliofanyiwa utu wao na, pia imani yao. Kanisa linapaswa kujifunza somo gumu kutoka yale yaliyopita, na kunahitajika kuwajibika kwa wale waliofanya vitendo hivyo na wale ambao waliruhusu unyanyasaji huo kutokea."
Hayo ni maneno katika taarifa ya makao makuu ya kanisa Katoliki mjini Vatican iliyosomwa na msemaji wa kanisa hilo Greg Burke. "Wale ambao wameathirika ndio anaowapa umuhimu wa kwanza, na kanisa linataka kuwasilikiza ili kuondoa maafa haya ya kutisha ambayo yanaharibu maisha ya watu wasio na hatia," taarifa ya Vatican imesema.
Kasisi Ricardo Ezzati akisimamia misa ya kwanza tangu kurejea kutoka Vatican mjini Santiago, baada ya makasisi wengi kujiuzulu kutokana na kashfa ya kuficha uhalifu wa kingono
Ripoti hiyo inafikiriwa kuwa yenye ufafanuzi mpana zaidi hadi sasa kuhusiana na unyanyasaji kingono katika kanisa nchini Marekani, tangu pale Boston Globe ilipofichua kwa mara ya kwanza kuwapo kwa mapadre wanaowalawiti watoto jimboni Massachusetts mwaka 2002.
Lakini wakati ripoti ya Jumanne imesababisha kufikishwa mahakamani mapadre wawili, mmoja wao akiwa amekiri kuwa na makosa, wengi wa wale wanaohusika wamekwisha fariki na uhalifu mkubwa zaidi ulitokea muda mrefu sana kuweza kuwafikisha mahakamani wahusika, maafisa wamesema.
Uchunguzi huo wa miaka miwili uliofanywa na jopo la wazee wa baraza la mahakama katika dayosisi zote isipokuwa mbili tu katika jimbo la Pennsylvania uliwaita mashahidi wengi pamoja na kurasa karibu nusu milioni cha rekodi za kanisa zilizokuwa na "madai mengi dhidi ya zaidi ya mapadre wahalifu 300."
"Kiongozi wa kanisa anatambua vizuri ni kiasi gani uhalifu huu unaweza kutikisa imani na mioyo ya waumini na kusisitiza wito wa kufanya juhudi kujenga mazingira salama kwa watoto na vijana pamoja na watu wazima ambao kuna uwezekano wakarubuniwa. Wahanga wafahamu kwamba Papa yuko upande wao. Wale walioathirika ni muhimu kwake na kanisa linataka kuwasilikiza ili kuondoa maafa haya ya kutisha ambayo yanaharibu maisha ya watu wasio na hatia."
Zaidi ya wahanga watoto 1,000 wametambuliwa, lakini idadi halisi inaweza kuwa maelfu," jopo hilo limekadiria. Wahanga wamesababishiwa hali ya fadhaa maishani, na kujiingiza katika madawa ya kulenywa, ulevi wa kupindukia na kutaka kujiua, jopo hilo limesema.
Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe
No comments
Post a Comment