Writen by
sadataley
7:47 AM
-
0
Comments
Wakristo wana unalazima na utume wa kuinjilisha kwa kuomba kwanza neema ya kuwa wasikilizaji wa Roho na ili kuweza kutoka nje kuonesha ukaribu kwa watu. Si kwenda kinadharia tu bali kwa njia ya matendo ya dhati. Huo ni uthibitisho wa maneno ya Baba Mtakatifu Francisko wakati wa misa yake ya asubuhi katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican tarehe 19 Aprili 2018, ambapo ameweza kueleza jinsi Roho inasukuma wakristo kuinjilisha.
Ili kuinjilisha ametumia maneno matatu kama ufunguo yaani kuamka, kukaribia, na kwenda katika maeneo ya hali halisi; Amesisitiza hayo kutokana na somo la Matendo ya Mitume iliyosoma ya siku, mahali ambapo Malaika wa Bwana alimwambia Filipo aamke na kwande saa sita katika njia ya Gaza huko Yerusalem, lakini njia hiyo ilikuwa ni jangwa.
Baada ya kifodini cha Mtakatifu Stefano, ilitokea kipeo kikubwa cha mateso ya kwa wakristu na mitume wakatawanyika karibia sehemu zote za mji wa Yuda na Samaria. Walakini katika upepo huo wa kuteswa, uliweza kutoa msukumo kwa mitume kwenda mbele zaidi. Kama upepo utawanyavyo mbegu, na kusambaza na kupanda, ndivyo ilivyojitokeza hata enzi zile za wakristo. Mitume walikwenda mbele zaidi kama mbegu ya Neno na kupanda Neno la Mungu. Kwa kutania Baba Mtakatifu amesema, leo hii tunaweza kusema ndipo ilizaliwa Propaganda Fide.
Kutokana na kuteswa kwao hadi upepo, mitume waliweza kuinjilisha na somo la siku ambalo limesomwa ni lenye uzuri mkubwa, ni sehemu kubwa ya uinjilishaji kwasababu ya kuhabarisha Bwana na ndiyo Bwana anataka namna hiyo kuinjilisha.Baba Mtakatifu anasistiza kuwa jinsi Roho Mtakatifu alivyomsukuma Filipo hata wakristo kuijilisha, ndiyo mtindo wa roho kuandaa hasa katika maneno matatu, amka, karibia na anzia katika hali halisi. Ni kwasababu baba Mtakatifu anathibisha uinjilishaji siyo mpango ambao umetengenezwa na waongofu wa dini ili kwamba waende wafanye uongofu kwa wengi, hapa na pale,hapana. Ni Roho Mtakatifu anaelekeza wapi tunapaswa kwenda na kupeleka Neno la Mungu, kupeleka jina la Yesu.
Hakuna uinjilishaji unaokaa katika sofa ili nzuri badala yake ni kuamka na kwenda nje daima. Kwenda ni tendo la mzunguko ambapo unalazimika kwenda na kusema Neno anathibitisha Baba Mtakatifu. Aidha amekumbuka jinsi gani watu wengi wanawake na wanaume waliweza kuacha nchi na familia zao, wakaenda nchi za mbali ili kupeleka Neno la Mungu, na mara nyingi walikuwa hawakujiandaa kimwili kukabiliana na magonjwa ya nchi zile, kwa maana hiyo vijana wengi walipoteza maisha na hata wengine ni mashahidi. Kwa njia hiyo walikuwa wote mashahidi wa uinjilishaji.
Ni muhimu kutembea daima katika njia ili kujinilisha lakini kuwa karibu na watu,hasa kuanzia hali halisi, kwa maana uinjilishaji unawezakana kwa njia ya mambo matatu lakini pia chini ya mwongozo wa Roho Mtakatifu, kwa maana bila Roho , tabia hizo tatu haisadii kitu. Ni Roho anayesukuma kuamka, kukaribia na kuanzia katika hali halisi!
Sr Angela Rwezaula
Vatican News
!
Vatican News
!
No comments
Post a Comment