Mali imeendelea kujikuta ikikabiliwa na shinikizo kutoka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutokana na kushindwa kutekeleza ahadi zake kuhusu utekelezaji wa mkataba wa amani ambapo Ufaransa na washirika wake wamesema wanataka kutambua wale wanaohusika na kutotekelezwa kwa mkataba huo.
Wadau wote wa makubaliano ya amani ambao wana uhusiano na makundi ya kigaidi au wafanyabiashara haramu wanalengwa na wanaweza kujikuta kwenye orodha ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa.
Mwishoni mwa mwezi Januari mwaka huu Ufaransa ilikaribisha kusainiwa kwa mkataba wa amani kwa ajili ya utekelezaji wa makubaliano ya amani lakini ilionya kuwa ikiwa kutakua na ucheleweshaji, vikwazo kadhaa vinaweza kuchukuliwa.
Serikali ya Mali na kundi la waasi la Azawad wananyooshewa kidole cha lawama kuhusika kwa njia moja ama nyingine kwa kushindwa kutekelezwa kwa mkataba wa amani nchini humo.
No comments
Post a Comment