Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Tandahimba Mkoani Mtwara kuhakikisha inadhibiti ongezeko la mimba kwa watoto wa shule ambapo takwimu zimeonyesha kupanda toka watoto 10 mwaka 2015 hadi 55 mwaka 2017.
Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi na Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba mkoani humo ambapo amesema ni lazima viongozi hao wasimamie nidhamu kwa kuwalinda watoto wa kike katika wilaya hiyo wasipate mimba ili waendelee na masomo.
"Hawa mabinti wote wamepotea, wamepoteza muelekeo. Nataka kuona mabadiliko mwaka huu 2018 hatutaki kusikia tuhuma, matatizo ya wanafunzi wetu kuacha shule kwa sababu ya mimba. Hawa vijana wote wanaohusika kuwapa mimba wanafunzi ni kuwakamata na kuwapeleka jela bila ya huruma", amesema Majaliwa.
No comments
Post a Comment