Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, March 1, 2018

Umoja wa Mataifa kurejea kufanya Uchunguzi


Kamati ndogo ya Umoja wa Mataifa kuhusu kuzuia vitendo vya utesaji na unyanyasaji 'SPT' imeamua kurejea nchini Rwanda baada ya kusimamisha uchunguzi huo Oktoba 2017, ingawa tarehe ya kurejea huko haijatangazwa mpaka hivi sasa.

Ziara hiyo iliamuliwa wakati wa kikao cha SPT kilichofanyika mjini Geneva Uswisi ambapo kamati hiyo vilevile imeamua kudurusu orodha ya mataifa ambayo hadi sasa yameshindwa kuunda chombo cha kitaifa kinachochunguza uzuiaji katika kipindi cha miaka minne baada ya kuudhinisha.

Kamati ndogo ya kuzuia utesaji-SPT inauwezo kufanya ziara yoyote ya kushtukiza kwa eneo lolote ambapo haki za watu zikiwa zinakiukwa katika nchi ambayo iliidhinisha itifaki ya mkataba wa kuzuia utesaji.

Vituo hivyo vinaweza kuwa ni magereza, vituo vya polisi, vituo vya kuwazulilia wahamiaji, vituo vya kuwashikilia watoto, vifaa vya kudodosa, na hospitali za watu walio na ulemavu wa akili.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment