Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, March 1, 2018

Rouhani: Iran haitafanya mazungumzo na yeyote kuhusu uwezo wake wa kujihami

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Iran haitaomba ruhusa kwa yeyote kwa ajili ya kutengeneza makombora na zana zake za kujilinda wala haitafanya mazungumzo na yeyote kuhusu suala hilo.
Rais Hassan Rouhani amewaambia raia wa Bandar Abbas huko kusini mwa Iran kwamba, Iran inakaribisha ushirikiano na nchi rafiki na jirani kwa ajili ya kulinda usalama wa eneo la Mashariki ya Kati na kwamba usalama wa eneo hilo hauhitajii madola ya kigeni. 
Ameashiria njama zilizofanywa na Marekani katika miezi ya hivi karibuni kwa ajili ya kutoa pigo kwa taifa la Iran na kusema: Marekani imetengwa katika jitihada zake za kutaka kutoa pigo kwa Iran na nchi zote za Ulaya na vilevile nchi nyingi duniani zimelaani harakati hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amepongeza misimamo ya Russia katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kushutumu hatua za Marekani na Uingereza na kusema: Jioni ya Jumatatu iliyopita Marekani ilitaka kutumia Baraza la Usalama kuilaani Iran kuhusiana na kadhia ya Yemen lakini imeshindwa kwa mara nyingine tena.
Rais Rouhani amewaambia walimwengu kwamba: Kama mnawajali watu wa Yemen msiipatie Saudi Arabia mabomu yanayofanya uharibifu na washinikizeni Wasaudia ili wafungue njia za kupeleka dawa na chakula kwa watu walioathiriwa na vita nchini humo. 
Amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendelea kusimama kidete kwa ajili ya kutetea maslahi yake na kwamba itaendelea kuheshimu makubaliano ya nyuklia ya JCPOA madamu nchi zilizotia saini mkataba huo zinayaheshimu. Amesisitiza kuwa kama nchi hizo makubaliano hayo Iran itakuwa na machaguo mengi.
  Parstoday  
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment