Klabu ya Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga, kupitia msemaji wake Dismas Ten amesema wamejipanga vizuri katika mchezo wao wa kesho dhidi ya Ndanda FC na kudai wanatoka vifua mbele ili waweze kujiweka sehemu nzuri.
Dismas ameeleza hayo asubuhi ya leo wakati alipokuwa yupo uwanjani akiwaangalia vijana wake wakiendelea kujiimarisha kwa kufanya mazoezi ya mwisho kabla ya mpambano wao huo wa VPL ambao utapigwa katika dimba la Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.
"Maandalizi yamekwisha fanyika ya kutosha na kitu pekee kwa sasa kinachotazamwa ni dakika 90 za uwanjani. Mwalimu Mwandamina amezungumza asubuhi ya leo na kusema ameiandaa timu vizuri lengo ni kuhakikisha tunapata matokeo ili tuweze kutengeneza nafasi nzuri zaidi katika msimamo wa ligi", amesema Dismas.
Timu ya Yanga itashuka dimbani kesho (Jumatano) ikiwa imeshika nafasi ya pili kibindoni kwa alama 37, Ndanda ikiwa nafasi ya 13 kwa pointi 18 huku Simba akiwa bado anaendelea kushika kilele kwa alama 45 mpaka sasa
No comments
Post a Comment