Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, February 27, 2018

Mfalme wa Morocco afanyiwa Operesheni ya Moyo


 Mfalme Mohammed VI wa Morocco Jumatatu amefanyiwa Ć“kwa ufanisiƶ operesheni ya moyo katika kliniki ya Paris, Ufaransa baada ya mapigo ya moyo kutokuwa ya kawaida, timu yake ya matibabu ilitangaza.

Madaktari hao katika taarifa, wamesema mfalme huyo mwenye umri wa miaka 54 alipata dalili za kusumbuliwa na moyo Januari 20.

"Tiba ya kuondoa mapigo yasiyo ya kawaida," au mrindimo usio wa kawaida ilifanyika kwa ufanisi kurejesha mapigo ya moyo ya kawaida.

Mfalme Mohammed, ambaye anatarajiwa kurejea kwenye shughuli zake za kawaida baada ya kipindi cha kupumzika kilichoamriwa na madaktari wake, ametawala Morocco tangu Julai 1999 alipofariki baba yake Mfalme Hassan,Aidha, Septemba mwaka jana alifanyiwa operesheni ya jicho jijini Paris.
BBC
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment