Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, February 25, 2018

Pep Guardiola agoma kusaini mkataba mpya Manchester City

Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola amegoma kuingia kandarasi mpya mpaka pale atakapo hakikisha anaipatia taji timu hiyo.

Guardiola ambaye alikuwa kocha wa Barcelona amekubali kandarasi mpya aliyopewa na City itakayo mfanya kusalia katika viunga vya Etihad mpaka mwaka 2021 lakini kwa upande wake amenuwia kutomwaga wino hadi atakapo iwezesha timu hiyo kunyakuwa taji.

Mkataba huo wenye thamani ya pauni  milioni 20 kwa mwaka utamfanya kocha huyo kuendelea kukinoa kikosi cha City ilhali ule wa sasa ukitarajiwa kufikia tamati mwishoni mwa msimu.

Mhispania huyo hakuwa na uhakika kama angekuwa zaidi ya miaka mitatu lakini hatimaye anasalia na kuendeleza ‘project’ yake City.

Habari kutoka ndani ya klabu hiyo zimesema kuwa, Guardiola anachohitaji ni kuhakikisha anatwaa taji lake la kwanza hapa kabla ya kusaini mkataba mpya na klabu.

Kikosi cha City kitakuwa na kazi kubwa wiki ijayo pale iatakapo kutana na Arsenal siku ya Jumapili katika kupigania taji la Carabao Cup katika dimba la Wembley.

Mmiliki wa klabu hiyo, Sheikh Mansour hana wasiwasi na Guardiola baada ya kukionyeshea dira kikosi cha timu hiyo huku ikiongoza ligi hiyo kwa wastani mzuri.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment