Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, February 25, 2018

Niyonzima aanza matibabu maalum India

Kiungo Haruna Niyonzima tayari ameanza matibabu ya mguu wake ambao umekuwa ukimsumbua, taarifa zinaeleza, Niyonzima ameanza matibabu hayo kwa kuchomwa sindano maalum na baada ya hapo atakuwa katika uangalizi maalum.

“Sindano hiyo ni maalum na madaktari watakuwa wakimfuatilia kwa uangalizi wao maalum,” kilieleza chanzo.

“Nimezungumza naye kwa kweli anaendelea vizuri na matumaini ni kuona anarejea haraka kabla ilivyokuwa inatarajiwa.”

Madaktari hao wa India wameshauri Niyonzima asifanyiwe upasuaji kama ilivyokuwa imeelezwa hapo awali.

Kiungo huyo nguli kutoka Rwanda hakupata nafasi ya kuonyesha cheche zake Simba aliyojiunga nayo akitokea Yanga baada ya kuumia mapema tu. Hali hiyo imemfanya akae nje ya uwanja kwa takribani miezi mitano sasa.

« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment