Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, June 18, 2017

Watoto wengi hawapati fursa ya kufurahia utoto wao na baba zao

Zaidi ya nusu au asilimia 55 ya watoto wa umri wa miaka 3 na 4 katika nchi 74 duniani ambao ni takribani watoto milioni 40 wana kina baba ambao hawachezi nao au kushiriki katika shughuli za elimu yao ya awali.
Hayo ni kwa mujibu wa uchambuzi uliotolewa Ijumaa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF.
Laurence Chandy mkurugenzi wa UNICEF wa kitengo cha takwimu, utafiti na sera amesema hali hii inadhihirisha kwamba kina baba wengi wanakabiliwa na changamoto ya kuwa na jukumu muhimu katika miaka ya awali ya watoto wao.

Ameongeza kuwa ni lazima kuondoa vikwazo vinavyowazuia kina baba hao kuwapa mazingira muafaka watoto wao ikiwemo upendo, muda wa kucheza nao, ulinzi na lishe bora.
UNICEF imetoa uchambuzi huu katika kuelekea siku ya baba duniani ambayo itaadhimishwa Jumapili Juni 18 katika nchi 80 ikiambatana na hashtag #EarlyMomentsMatters ikichagiza kina baba kuwa na wajibu mkubwa kwa watoto wao.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment