Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, June 17, 2017

Waliofariki mkasa wa moto London wafika 30

Malkia Elizabeth

Haki miliki ya pichaPA
Image captionMalkia Elizabeth ametembelea kituo cha misaada ambacho kinawasaidia manusura wa mkasa huo wa moto.
Polisi wamethibitisha kwamba idadi ya watu waliofariki kutokana na mkasa wa moto katika jumba la Grenfell Tower magharibi mwa London imefikia 30.
Bado kuna watu wengi ambao hawajulikani walipo.
Kamanda wa polisi Stuart Cundy amesema inaaminika kwamba idadi ya waliofariki huenda ikaongezeka, lakini kwa sasa ni vigumu sana kubaini ni watu wangapi ambao hawajulikani walipo.
Hii ni kwa sababu huenda jamaa wamepiga ripoti mara kadha, kila mmoja kivyake, kuhusu jamaa zao ambao hawajui waliko.
Amesema polisi watachunguza kubaini iwapo kulitendwa makosa ya jinai.
Malkia Elizabeth na Mwanamfalme William walitembelea kituo cha misaada ambacho kinawasaidia manusura wa mkasa huo wa moto.
Grenfell TowerHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Waziri Mkuu Theresa May naye amezungumza na majeruhi hospitalini, baada yake kukosolewa kwamba hakuzungumza na wakazi alipozuru eneo la mkasa Alhamisi.
Moto huo ulizuka mwendo wa saa moja usiku, usiku wa kuamkia Jumatano.
Grenfell TowerHaki miliki ya pichaEPA
Image captionMaafisa wamesema hawatarajii kuwapata manusura

BBC

« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment