Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, June 17, 2017

Wabunge wabanwa

Dodoma. Bunge limeweka taratibu mpya zitakazolazimisha wabunge wanaowasilisha ushahidi wakati wakichangia mijadala, kuhakikisha nyaraka zao zinahakikiwa na kuthibitishwa na mwanasheria, kabla ya kukabidhi mezani kwa Spika wa Bunge.

Kauli hiyo imekuja siku moja baada ya mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea kuwasilisha nyaraka zinazoonyesha barua ya mwaliko wa mbunge wa Lupa (CCM), Victor Mwambalaswa aliopewa na viongozi wengine wa Shirika la Umeme (Tanesco).

Mwaliko huo kwa mujibu wa Kubenea ambao ulitolewa wakati Mwambalaswa akiwa makamu mwenyekiti wa bodi ya shirika hilo, ulikuwa ni kwa ajili ya kusaini mkataba wa kampuni ya kufua umeme kwa kutumia upepo mkoani Singida.

Mwenyekiti wa Bunge, Najma Giga alisema wakati wa kuahirisha kikao cha Bunge jana mchana kuwa amepata maelekezo kutoka kwa Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah akiwataka wanaowasilisha nyaraka za ushahidi wa hoja zao kufuata utaratibu huo mpya.

“Kwa nyakati tofauti huku bungeni, waheshimiwa wabunge wamekuwa wakitoa nyaraka za ushahidi wa mambo wanayochangia na wakati mwingine kuwasilisha nyaraka hizo,” Najma alimnukuu Dk Kashililah.

“Ili kuleta uhalali wa nyaraka hizo kwa mujibu wa Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge na kanuni za Bunge, utaratibu ufuatao unatakiwa kufuatwa kwanza.

“Nyaraka zinazofikishwa mezani zinatakiwa kusainiwa kila ukurasa na mbunge anayewasilisha.”

Pia, Najma alisema nyaraka za wabunge hao zinatakiwa kuwa zile zilizohakikiwa na kuthibitishwa na mwanasheria kuwa ni nakala halisi.

Alisema kutokana na utaratibu huo, Kubenea ametakiwa afike ofisini kwa katibu wa Bunge ili atimize masharti hayo.

Kubenea alipoulizwa baadaye nje ya ukumbi wa Bunge, alisema utaratibu huo mpya haumuhusu na kwamba anasubiri Bunge limpe maagizo hayo kwa njia ya maandishi.

Kwa sasa, Bunge linaendelea na mjadala wa hotuba ya bajeti ya mwaka 2017/18 ambayo iliwasilishwa bungeni Alhamisi iliyopita. Bajeti hiyo ni ya Sh31.7 trilioni.    
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment