Aliyewahi kuwa Makamu Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Athumani Nyamlani, ameamua kugombea tena urais wa shirikisho hilo.
Taarifa za uhakika kutoka kwa rafiki wa karibu wa Nyamlani zinaeleza, atachukua fomu leo saa 5 asubuhi kugombea nafasi hiyo dhidi ya Jamal Malinzi.
Kabla ya Nyamlani kuchukua fomu, tayari watu wanne wamejitokeza kuwania urais ambao ni Malinzi,
Imani Madega, Wallace Karia na Fredrick Masolwa.
Nyamlani atakuwa anagombea nafasi hiyo kwa mara ya pili baada ya kugombea kwa mara ya kwanza na kushindwa na Malinzi ambaye anaonekana kutofanya vizuri wakati wa miaka yake minne.
Nyamlani ndiye alikuwa injini ya utendaji wakati wa uongozi wa Leodeger Tenga ambao ulileta mabadiliko makubwa katika uongozi wa soka nchini.
No comments
Post a Comment