Writen by
sadataley
4:18 PM
-
0
Comments
John Kelly
Wizara ya Ulinzi wa Ndani ya Marekani imesitisha program ya uhamiaji iliopendekezwa wakati wa utawala wa Obama.
Program hiyo ilikuwa na nia ya kuzuia kuondolewa hapa Marekani kwa wazazi ambao watoto wao walizaliwa hapa nchini na ambao ni wakazi wa kudumu nchini.
Katika taarifa iliotolewa Alhamisi, wizara hiyo imesema kuwa waziri wake John Kelly ametia saini ya kubatilisha program hiyo maarufu kama DAPA akisema kuwa hakuna njia mwafaka ya kisheria ya kuiendeleza.
Rais aliyeondoka madarakani Barack Obama alitangaza program hiyo 2014 lakini ikapingwa kwenye mahakama ya serikali baada ya majimbo 26 kudai kuwa Obama alichukua hatua kinyume na mamlaka yake.
Pia ilidai kuwa program hiyo ilikuwa na dhamiri yakulinda kundi fulani la wahamiaji wasio halali na wanaoishi hapa Marekani.
Hatua dhidi ya wahamiaji wasio halali ilikuwa mojawapo ya ajenda muhimu kwenye kampeni za Rais Donald Trump.
VOA Swahili
Social Buttons