Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, June 24, 2017

BALOZI MIGIRO AMTUNUKU KIJANA ALIYESHINDA PICHA ZA KIMATAIFA


  
 TUMEZOEA kuwaita wenye hali hii “taahira” – neno la asili ya Kiarabu lenye maana “mtu asiye sawa” (wazimu, chizi, bwege, nk). Ila sahihi ni “mtindio ubongo” – kwa Kiingereza “Down Syndrome”....
Baadhi ya taswira zake ni : kufikiri na kuzungumza taratibu, kigugumizi, mwili mfupi, utofauti wa tambo la kichwa, vidole vya mikono na miguu, nk. Mbali na kuwanyanyapaa, jamii zetu Afrika bado hazitambui umuhimu wa kuendeleza wenye ulemavu. Mwaka huu kijana wa miaka 18, Samwel Mwanyika, mwenye “Mtindio Ubongo “ (Down Syndrome) alikuwa mshindi wa kimataifa wa upigaji picha. Balozi wetu Uingereza Mheshimiwa Asha-RoseMigiro akaeleza: “Wametoka vijana wengi kwenye nchi zilizoendelea, wengine wamemzidi umri...tena wenzetu huwa na mipango maalum ya kuwapa mbinu mbalimbali,...sasa huyu wa familia ya kawaida tu ya Kitanzania ambapo bado hatujaweka miundo mbinu kama walivyoweka huku, picha yake imeshinda...” Mwasisi wa kujitolea wa shirika la Mtindio Ubongo (Pearl of People with Down Syndrome) , Mony Teri Pettite na wazazi wake Samwel, Philip Mwanyika na Sophie Mshangama, walikutana na Balozi Migiro na kupongezwa Ijumaa iliyopita. Afisa Utawala Ubalozini, Rose Kitandula , pia alikuwepo. 
 Samwel Mwanyika na picha ailiyonyakua tuzo la kimataifa la Stephen Thomas, mjini London. 
Balozi Migiro akimvika Samwel Mwanyika bendera ya taifa, alipowakaribisha na familia ofisini    
Afisa Utawala Ubalozini, Rose Kitandula na Mheshimiwa Balozi wakiwa na Samwel Mwanyika na mwenzake mwenye “Mtindio Ubongo” (Down Syndrome), Penina Haika Petitt. 
 Picha ya pamoja . Toka kushoto, Mjomba wake Sam, Hassan Mshangama, Mama Sam, Sophie Mshangama, Mony Teri Pettite, Penina Haika Pettite, Balozi Migiro, Sam Mwanyika, Rosa Kitandula (Afisa Utawala Ubalozini), na Philip Mwanyika (baba wa mshindi) 
Balozi Migiro akiwasikiliza wageni na kuwapongeza
Balozi Migiro akizungumza na Mony Teri Petitte mwasisi wa “Pearl of People with DownSyndrome” anayejitolea kuendesha Jumuiya ya Watanzania wenye Mtindio Ubongo (Down Syndrome). 
Tuzo ya Stephen Thomas

 
Sophie Mshangama, mama mzazi wa mshindi akizungumzia harakati za malezi.
Kuona zaidi -Pitia “Kwa Simu Toka London” https://www.youtube.com/channel/UCtVEe3zlUtuF6pTbn_OK8JQ
Habari na Picha za Freddy Macha
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment